Mtoto wa miaka 9 aweka rekodi kwa kuwa mtu mdogo zaidi kufika kilele cha mlima Aconcagua wa Argentina

Mvulana wa miaka 9 kutoka Kusini mwa California, Marekani ameweka rekodi mpya kwa kuwa mtu mwenye umri mdogo kuwahi kupanda na kufika kweny... thumbnail 1 summary
Mvulana wa miaka 9 kutoka Kusini mwa California, Marekani ameweka rekodi mpya kwa kuwa mtu mwenye umri mdogo kuwahi kupanda na kufika kwenye kilele cha mlima Aconcagua ulioko nchini Argentina.

Tyler akiwa kileleni
Tyler akiwa kwenye kilele cha mlima Aconcagua

Mtoto huyo aitwaye Tyler Armstrong na baba yake walifanikiwa kufika kwenye kilele cha mlima huo wenye urefu wa futi 22,841, siku ya Christmas mwaka huu.

Aconcagua mountain
Aconcagua Mountain

Kwa mujibu wa New York Daily News, ni asilimia 30 tu ya watu 7,000 wanaopata vibali vya kuupanda mlima Aconcagua ambao hufanikiwa kufika kileleni, pia zaidi ya watu 100 wamewahi kuripotiwa kufariki wakijaribu kuupanda mlima huo..

Tyler na baba yake
Tyler na baba yake baada ya kushuka kutoka mlimani

Hata hivyo haikuwa kazi rahisi kwa Tyler kufanikisha safari hiyo, sababu alianza maandalizi ya kupanda mlima huo zaidi ya mwaka mzima uliopita, ambapo alikuwa akifanya mazoezi mara mbili kwa siku kwa mwaka mzima na nusu.
Rekodi iliyokuwepo kwa mtu mwenye umri mdogo zaidi kuwahi kupanda mlima huo iliwekwa na Matthew Moniz ambaye alikuwa na miaka 10 wakati alipofanikiwa kufika kilele cha mlima huo mwaka 2008.
Tyler pia amewahi kupanda mlima Kilimanjaro ulipo Tanzania alipokuwa na miaka 8.
Source: NY Daily News imehaririwa na Bongo5