Mhe.
Abdulkarim Shah Mbunge wa Mafya kwa tiketi ya CCM akiongozana na ujumbe
wake wa Tanzania Tourist Board (TTB) na Tanzania National Parks
(TANAPA) walipowasili Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani, Washington,
DC kwenye chakula cha jioni walipokaribishwa Ubalozini hapo siku ya
Alhamisi June 19, 2014
.
Wengine waliokaribishwa ni Jumuiya ya Watanzania DMV, Kamati ya
maandalizi ya sherehe ya Vijimambo, Katibu wa Jumuiya New York alikuwepo
lakini chini ya kivuli cha Miss Tanzania USA Pagent chini ya Ma Winny
Case. Ujumbe wa TTB na TANAPA ulialianzia New York na wapo nchini
Marekani kwa ajili ya kutangaza Utalii wa Tanzania kwa kufanya
mazungumuzo na watu mbalimbali vikiwemo vyombo vya habari kwa ajili ya
matangazo na kupata mbinu mbalimbali za kupambana na ujangili wa mali
asili na hatimae kuutokomeza kabisa.
Mjini
New York walipata fulsa ya kufanya mazungumuzo na CNN International na
Local na vyombo vingine vya habari yakiwemo magazeti kwa ajili ya
kutangaza utalii na mali asili kitu ambacho kinaendelea pia kufanywa na
Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani chini ya Balozi Mhe. Liberata
Mulamula na kufanya nchi ya Marekani kuongoza hivi sasa katika kupeleka
watalii wengi nchini Tanzania. Katika picha Mhe. Abdulkarim akisalimiana
na Rais wa Jumuiya ya Watanzania DMV Bwn. Idd Sandaly.
Mkurugenzi
mkuu wa Tanzania National Parks (TANAPA) Bw. Allan Kijazi akisalimia na
mjumbe wa bodi ya wadhamini wa Jumuiya ya Watanzania DMV, Bw. Ulotu
wakati alipokuwa akiwasili kwenye Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani
waliokaribishwa chakula cha jioni na Ubalozi wa Tanzania , Washington,
DC.
Mkurugenzi
masoko wa Tanzania Tourist Board (TTB) Bi. Teddy Mapunda akisalimiana
na mjumbe wa bodi ya wadhamini wa Jumuiya ya Watanzania DMV, Bwn. Ulotu
wakati alipokuwa akiwasili kwenye Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani
waliopokaribishwa chakula cha jioni na Ubalozi wa Tanzania , Washington,
DC. Nyuma ya Bi. Teddy Mapunda ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tanzania
Tourist Board Bi. Devota Mdachi akisalimiana na Mwambata wa Jeshi wa
Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani, Colonel Adolph Mutta.
Balozi
wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula akifanya utambulisho
wa wageni na maafisa na wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania nchini
Marekani na baadae kuwakaribisha chakula cha jioni.
Balozi
wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula akijipatia chakula,
wengine katika picha ni Mariam Mkama, Edward Taji, Afisa Suleiman Saleh,
Mercy Dachi na Rose Mzirai Commodore.
Kutoka
kushoto ni Mrs Esther Zoka Mhe. Abdulkarim Shah, Mkurugenzi Mkuu wa
TANAPA, Bw. Allan Kijazi wakiendelea kujipatia chochote kwenye chakula
cha jioni walichakaribishwa na Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani.
Wageni waalikwa wakiwa na mwenyeji wao Balozi Liberata Mulamula kwenye chakula cha jioni.
Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula akiongea jambo huku wageni wake wakiendelea na chakula cha jioni.
Mhe.
Abdulkarim Shah (watatu toka kushoto) akiwa na mwenyeji wake Mhe.
Liberata Mulamula katika picha ya pamoja na wageni waalikwa kwenye
mkaribisho wa chakula cha jioni kwenye Ubalozi wa Tanzania nchini
Marekani, jijini Washington, DC.
Mhe.
Balozi Liberata Mulamula katika picha ya pamoja na familia ya Zoka
kutoka kushoto ni Andrew Mgendi Zoka, Mrs Esther Mgendi Zoka na kulia ni
Mr. Jacky Mgendi Zoka.
Picha ya pamoja. Picha zaidi BOFYA HAPA