Tanzania yapata msaada wa magari maalumu 50 ili kuongeza nguvu katika mapambano dhidi ya ujangili

Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii imekabidhiwa msaada wa magari maalumu 50 pamoja na vifaa vya vingine 417 ... thumbnail 1 summary
Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii imekabidhiwa msaada wa magari maalumu 50 pamoja na vifaa vya vingine 417 na Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China ili kuongeza nguvu katika mapambano dhidi ya Ujangili.

Katika makabadhiano hayo , Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China imetoa magari 50 yenye thamani ya bilioni 2.6 yakiwemo magari yenye matairi matatu yenye uwezo ya kutembea sehemu yoyote ya pori hata mahali pasipo na barabara ili kuweza kuwasaidia Askari wanyamapori kukabiliana na majangili watakaothubutu kutoroka.

Mbali ya magari hayo , China imetoa vifaa maalumu vya kukagua makontena ili kubaini endapo yamebeba nyara za Serikali ambapo kwa awamu hii ya kwanza vifaa hivyo vitaanza kutumika katika Bandari ya Dares Salaam.

Akizungumza jana jijin Dares Salaam muda mfupi mara baada ya makabidhiano hayo , Waziri wa Maliasili na Utalii. Mhe. Lazaro Nyalandu alisema magari hayo maalumu yatasaidia Askari wanyamapori kumudu kazi kwa kushirikiana na vyombo vya usalama katika kuwakamata majangili popote walipo.

Amesema Serikali ya Jamhuri ya watu wa China imeonesha njia kwa Mataifa makubwa kwa kuisaidia Tanzania kupambana na Ujangili, ‘’ Serikali ya Tanzania haina mzaha na mtu yeyote anayejihusisha na Ujangili, ‘’ Mhe, Nyalandu alisema.

‘’Magari haya tuliyokabidhiwa leo yatapelekwa moja kwa moja kwenye maeneo ya kazi na kamwe hayatabaki hapa kwa ajili ya matumizi ya maofisa,, Huu ni mpango endelevu wa vitendea kazi kwa ajili ya Askari wanyamapori ili kuwasaidia kumudu kazi ya kupambana na majangili’’ Mhe. Nyalandu alisema.

‘’Serikali inatoa onyo kwa wananchi wanaowahifadhi majangili na wanaoshirikiana na majangili ninawasihi waache mara moja’’ Mhe. Nyalandu alisisitiza

Mhe. Nyalandu amesema vita dhidi ya Ujangili ni vita ya kidunia hivyo Tanzania imekuwa ikishirikiana na Askari wa Kimataifa ( Interpol) pamoja na kupata msaada kutoka kwa mataifa makubwa katika kutokomeza mtandao wa Ujangili.

Akizungumza katika makabidhiano hayo. Balozi wa China nchini Tanzania Bw. Lu Youqing amesema nchi yake itaendelea kuisadia Tanzania katika vita dhidi ya Ujangili kutoka na tatizo kubwa la ujangili lililopo licha ya jitihada kubwa zinazofanywa na Serikali ya Tanzania.

‘’Tumeamua kuongeza nguvu katika mapambano dhidi ya Ujangili kutokana na si Tanzania tu inayoathirika na tatizo la Ujangili bali ni tatizo linaloathiri hata mataiafa makubwa Makubwa ikwemo sisi’’ Balozi wa China nchini Tanzania, Bw. Lu Youqing alisema.

Alisema wameanza kuonyesha kwa vitendo kushirikiana na Tanzania katika vita dhidi ya Ujangili kwa kutoa vifaa vya kisasa ambavyo vitawawezesha Askari wanyamapori kuweza kuwasiliana kwa urahisi katika maeneo yao ya kazi.