SERA YA TANZANIA YA UTALII ENDELEVU YAPONGEZWA.

Mkurugenzi wa Kituo cha Biashara cha Tanzania, London, Bwana Yusuf Kashangwa, akihutubia kwenye Semina kuhusu Utalii, Tanzania.  Semin... thumbnail 1 summary
Mkurugenzi wa Kituo cha Biashara cha Tanzania, London, Bwana Yusuf Kashangwa, akihutubia kwenye Semina kuhusu Utalii, Tanzania.  Semina ambayo ilifanyika siku ya Jumamosi Tarehe 13 October 2012 katika mji wa Redditch, nchini Uingereza. Semina ambayo ilihudhuriwa na Wataalam na Wawakilishi mbalimbali kutoka katika sekta ya Utalii, iliyoandaliwa na Britain Tanzania Society kwa kushirikiana na Redditch One World Link (ROWL), Uingereza.
Mkurugenzi, Bwana Yusuf Kashangwa, akimkabidhi Mstahiki Meya wa Mji wa Redditch, Bwana Allan Mason, zawadi kutoka Tanzania, kama heshima na kuthamini mchango wa Ushirikiano mwema kati ya Mji wake wa Redditch na Tanzania. Mstahiki Meya, Allan ameahidi kuetembelea Tanzania Mwakani.
Baadhi ya Wawakilishi katika Semina hiyo pichani, wakisikiliza kwa makini Mada mbalimbali zikitolewa kuhusu Utalii, Tanzania
Wawakilishi kutoka sekta mbalimbali ya Utalii, waligawanywa kwenye makundi, kujadili changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo katika kusaidia kukuza na kuboresha Utalii Tanzania
Mkurugenzi wa Kituo cha Biashara, London, Bwana Yusuf Kashangwa (kwanza kushoto), akiwa kwenye Picha ya pamoja na Mstahiki Meya wa Mji wa Redditch, Bwana Allan Mason, mara baada ya kumalizika kwa Semina hiyo. Wa kwanza kulia, Bwana Mohamed, afisa kwenye Kituo cha Biashara, London.
---
 
Hayo yalikuwa ni maoni ya wataalamu mbalimbali wa masuala ya utalii, mazingira na maendeleo waliyoyatoa kwenye semina iliyoandaliwa mjini Redditch kujadili Hali ya utalii nchini Tanzania. 

Semina hii iliandaliwa kwa ushirikiano wa Redditch One World Link (ROWL) na Britain-Tanzania Society (BTS), ilifanyika siku ya Jumamosi Terehe 13 October 2012, na mada kadhaa ziliwasilishwa na kujadiliwa na wana semina wapatao 150 hivi. Mgeni rasmi katika semina hiyo alikuwa ni Mstahiki Meya wa Mji wa Redditch, Bwana Allan Mason.
Mji wa Redditch kupitia Shirika lisilo la kiserikali la Redditch One World Link (ROWL) una uhusiano wa kirafiki na mji wa Mtwara nchini Tanzania tangu mwaka 1985.

Baada ya hotuba ya makaribisho ya mgeni rasmi, Mkurugenzi wa Kituo cha Biashara cha Tanzania Ubalozini London, alikuwa wa kwanza kuwaeleza wana semina juu ya vivutio mbalimbali vilivyoko nchini Tanzania na pia juu ya sera ya Utalii endelevu inayotekelezwa na serikali ya Tanzania. Aligusia vipengele muhimu vya sera hiyo kuwa ni kuongeza mchango wake katika pato la Taifa, kujali maslahi ya Taifa , ya watu wake, kuhifadhi mazingira na rasilimali nyinginezo kupitia mikakati na  mipango mbalimbali na kusimamia utekelezaji wake na kwa kuwashirikisha  wadau wote bila ya kusahau wananchi wa kawaida kokote waliko katika maeneo yenye vivutio asilia vya kitalii .


Watoa mada wengine walikuwa ni Bw. Nigel Nicoll, Mkurugenzi Mkuu wa African Travel and TourismAssociation (ATTA) aliyeongelea juu ya changamoto wanazokumbana nazo wadau wa utalii, Mark Watson, Mtendaji Mkuu wa Tourism Concern aliyeongelea juu ya utalii, mazingira na kujali maadili. Bi Catherine Brenan alielezea uzoefu alioupata  baada ya kupanda mlima Kilimanjaro, akichangisha fedha za kumalizia jengo la shule.
Kama ilivyo BTS, ROWL hujihusisha na kukuza mahusiano  ya kirafiki, kubadilishana uzoefu  na kusaidia nyanja mbalimbali za maendeleo, kijamii , kiuchumi na kiutamaduni