Bodi ya utalii Tanzania yaratibu na kuongoza msafara kupanda Mlima Kilimanjaro

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania – TTB anaongoza timu ya watu saba miongoni mwao wakiwemo wafanyakazi wa Bodi ya... thumbnail 1 summary
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania – TTB anaongoza timu ya watu saba miongoni mwao wakiwemo wafanyakazi wa Bodi ya Utalii Tanzania kupanda mlima Kilimanjaro ambao pia ni mrefu kuliko yote barani Afrika na ambao pia ni miongoni mwa maajabu saba ya asili barani Afrika.
TTB YARATIBU NA KUONGOZA MSAFARA KUPANDA MLIMA KILIMANJARO
Mkuu wa kitengo cha utalii cha Hifadhi ya Taifa ya Kilimanjaro (KINAPA) Bw. Mombo akitoa 
maelezo kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TTB Balozi Charles Sanga (kushoto) na
Meja Jenerali mstaafu Gimonge kuhusu njia mbalimbali zinazotumika katika kupanda mlima
Kilimanjaro muda mfupi kabla ya Balozi Sanga kuanza kuongoza msafara wa kupanda mlima


Msafara huu ujulikanao kama Uhuru Expedition ambao ni mahsusi kwa ajili ya kuadhimisha miaka 52 ya uhuru umeratibiwa na kufadhiliwa na Bodi ya Utalii Tanzania umeanza kupanda mlima Kilimanjaro tarehe 6/12/2013 umeanza kupanda mlima Kilimanjaro tarehe 6/12/2013 umeanza kupanda mlima Kilimanjaro tarehe 6/12/2013 kupitia njia ya Marangu na unatarajia kumaliza zoezi hilo tarehe 10/12/2013.

TTB YARATIBU NA KUONGOZA MSAFARA KUPANDA MLIMA KILIMANJARO
Msafara wa Uhuru expedition katika picha ya pamoja na waongoza wapamda mlima
muda mfupi kabla ya kuanza kupanda mlima Kilimanjaro kupitia njia ya Marangu

Msafara huo wenye jumla ya wapandaji mlima saba (7) ambapo kutoka TTB ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Balozi Charles Sanga, Bw. Musa Kopwe na Bw. Hillary Mushi. Aidha katika msafara huo yumo pia Meja Jenerali mstaafu Gimonge, Bley Mayo, Bibi Lidya Kayuni na Bw. Joan Mwamlima wote kutoka Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.

TTB YARATIBU NA KUONGOZA MSAFARA KUPANDA MLIMA KILIMANJARO
Mwenyekiti wa TTB Balozi Sanga (wa pili kushoto)sambamba na wapanda mlima 
expedition wakichanja mbuga kuelekea kituo cha Mandara.

Hii ni mara ya pili kwa Bodi ya Utalii Tanzania kuratibu msafara huu kwa lengo la kuadhimisha siku ya uhuru wa Tanzania Bara. Mara ya kwanza kwa TTB kufadhili Uhuru Expedtion ilikuwa ni mwaka jana ambapo pamoja na TTB Kampuni nyingine kama ya bia ya Serengeti ilijitoleza pia kudhamini Msafara huo wa Uhuru ulioongozwa na aliyekuwa mkuu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Jenerali mstaafu George Waitara.