Wabunge Tanzania watakiwa kujitokeza kutahiriwa, waombwa kuiga mfano wa Zimbabwe

Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wameombwa kuiga mfano wa Wabunge wa Zimbabwe kwa kujitokeza kutahiriwa ikiwa ni hatua moja w... thumbnail 1 summary
Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wameombwa kuiga mfano wa Wabunge wa Zimbabwe kwa kujitokeza kutahiriwa ikiwa ni hatua moja wapo ya kupambana ana maambukizi ya virusi vya Ukimwi nchini.

Wito huo umetolewa leo Bungeni Mjini Dodoma na Mbunge wa Konde (CUF) Khatib Haji ambapo alisema kuwa mfano huo ni wa kuigwa na Wabunge wote ambao hawajatahiria wanapaswa kufanya hivyo ili kuwahamasisha wananchi wao.

Wiki iliyopita Wabunge nchini Zimbabwe wametahiriwa kama moja wapo ya hatua zao ya kukabiliana na kusambaa kwa virisi vya Ukimwi nchini humo
Njee ya majengo ya bunge mjini Harare , kulijengwa zahanati ndogo kwa sababu ya shuhuli hizo za kuwapasha wabunge tohara.

Blessing Chebundo, ambaye ni mwenyekiti wa wabunge wanaopambana na Ukimwi amesema nia yake hasa ya yeye kuamua kupashwa tohara ni kuchochea wanaume nchini Zimbabwe kutairiwa.