Demaco yasambaza matrekta 110 mikoani

na Mwandishi wetu KAMPUNI ya Developing Mechanised Agriculture LTD (Demaco), imesambaza matrekta 110 katika mikoa minne ya Morogoro, Ir... thumbnail 1 summary

na Mwandishi wetu

KAMPUNI ya Developing Mechanised Agriculture LTD (Demaco), imesambaza matrekta 110 katika mikoa minne ya Morogoro, Iringa, Singida na Mbeya tangu mwaka 2007.

Mkurugenzi wa Demaco, Kaya Kazema, alisema kuwa walishirikiana na Catic Africatic Limited, Suma JKT, Zana Bora Limited na Noble Motors Ltd.

Kwamba katika kipindi hicho Mkoa wa Morogoro ulipata matrekta 80 yaliyokopeshwa kwa wakulima kuboresha kilimo na kufikia azima ya Kilimo Kwanza.

Alisema matrekta hayo yakiwamo madogo aina ya Power Tiller yaliyouzwa kwa kati ya sh milioni tano hadi 62, yamefanikisha kupanua kilimo kwa mkulima mdogo.

“Hata hivyo tunatarajia kutoa matrekta kati ya 200 hadi 400 kwa kushirikiana na shirika za uzalishaji la Jeshi la Kujenga Taifa (Suma JKT) katika baadhi ya mikoa ya hapa nchini kupanua soko na kuboresha kilimo," alisema.

Aliitaja mikoa itakayonufaika kuwa ni Mbeya, Iringa, Rukwa, Katavi, Iringa, Kigoma, Ruvuma, Dodoma, Singida na Morogoro utakaopata matrekta 70.

Kuhusu changamoto zinazowakabili, alisema ni pamoja na hali mbaya ya hewa kwa mkulima kushindwa kufikia lengo la uzalishaji na hivyo kushindwa kurejesha mikopo kwa wakati hivyo kuongeza muda hadi kufikia zaidia ya miaka minne.

Chanzo: Tanzania Daima