Wizara kuanzisha kitengo kudhibiti mazingira

na Shehe Semtawa WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Dk. Trezya Huvisa, amesema wizara hiyo inatarajia kuanzisha Kiten... thumbnail 1 summary



na Shehe Semtawa
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Dk. Trezya Huvisa, amesema wizara hiyo inatarajia kuanzisha Kitengo cha Polisi kitakachosimamia utunzaji wa mazingira na kuwakamata wale wote wataochangia kuyaharibu.
Huvisa alitoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam jana, alipozungumza na waandishi wa habari, kuhusu maadhimisho ya Siku ya Mazingira itakayofanyika Machi 3 kwenye viwanja vya Tanganyika Parkers.
Alisema kitengo hicho kitafanya kazi ya kuwadhibiti watu wanaofanya uharibifu wa mazingira kwa kushirikiana kwa karibu na jamii ambayo inawatambua baadhi yao.
“Ni vema tunapoadhimisha siku hii tutafakari kwa kina changamoto mbalimbali zinazochangia uharibifu mkubwa wa mazingira,” alisema.
Alisema siku hiyo imetengwa kwa lengo la kukumbushana juu ya umuhimu wa kutunza na kuhifadhi mazingira barani Afrika.
Aidha, alimtaka kila mmoja kutumia fursa hiyo kwa kuelimisha na kukumbushana kuhusu wajibu wa kuyatunza mazingira kwa manufaa ya kila mtu na vizazi

Chanzo: Tanzania Daima


Una taarifa, picha za usafiri wa anga, mazingira, maliasili na utalii? tutumie kupitia kingkahindi@gmail.com