Kikosi cha ujangili chazuia jaribia la wakulima la kuwaua wafugaji tisa waliokuwa wamewateka

KIKOSI dhidi ya ujangili kanda ya Mwanza kwa kushirikiana na polisi wa vituo vya Nyamboge na Nzera wilayani Geita wamewakamata wakulima 50 ... thumbnail 1 summary
KIKOSI dhidi ya ujangili kanda ya Mwanza kwa kushirikiana na polisi wa vituo vya Nyamboge na Nzera wilayani Geita wamewakamata wakulima 50 waliokuwa wamewateka wafugaji sita wa ng'ombe kwa lengo la kuwaua.
Tukio hilo limetokea juzi majira ya asubuhi kufuatia kuibuka kwa vurugu kati ya wakulima na wafugaji kugombania maeneo kwenye hifadhi ya Msitu wa Ruande wilayani Geita.
Wakulima hao wakiwa na silaha za jadi kama mapanga,fimbo,visu na shoka wamekamatwa baada kukutwa wakiwa wamewazingira wafugaji hao wakitaka kuwaua kwa kuwachinja shingo.
Hatua hiyo inatokana na wakulima kuwatuhumu wafugaji kwamba wamekuwa wakiwachongea serikalini wafukuzwe kwenye hifadhi hiyo ili wasiendelee na kilimo.
Kiongozi wa kikosi hicho cha kuthibiti ujangili,Samweli Mwita ambaye ni ofisa wanyama pori wilaya ya Nyang'hwale mkoani Geita amesema awali walipata taarifa kutoka kwa wasamalia wema kwamba kuna wafugaji wametekwa na kundi kubwa la wakulima wanataka kuuawa.
Amesema kikosi hicho ambacho kilikuwa kinaendelea na doria ya kuwasaka fisi kililazimika kwenda eneo la tukio kisha kufyatua risasi hewani kuwathibiti wakulima ambao walikuwa wamewazingira wafugaji wasitawanyike,hatua iliyofanikisha kuwatia nguvuni watu hao.

Kikosi hicho kipo katika vijiji vinavyozunguka hifadhi hiyo kikiendelea na doria ya kuwasaka fisi ambao wamekuwa tishio kwa maisha ya watu hasa watoto baada ya kutapakaa kwenye makazi ya watu kutokana na uharibifu wa mazingira ndani ya hifadhi hiyo.