Ndiyo kwanza nimemaliza kukwea Mlima Kilimanjaro katika mwaka wa 6 wa The Mwalimu Nyerere/Mt. Kilimanjaro Charity Climb kuchangisha pesa kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa shule iliyopo kwenye kijiji cha Kichalikani, wilayani Mkinga, mkoa wa Tanga.
Kwenye kilele cha Mlima Kilimanjaro, mita 5,895 juu ya usawa wa bahari na sehemu iliyo juu kuliko zote katika bara la Afrika, kutoka kushoto: Pius Yahoo, muongozaji wetu; E. Gassana; mwandishi wa blogu hii; na Musa Juma, muongozaji msaidizi.
Wakazi wa kijiji cha Kichalikani walianza ujenzi wa shule mwaka 2009 kwa kutumia sehemu ya ushuru uliokusanywa kwenye soko la samaki. Baada ya kuona jitihada hizi, Saidi Masimango, aliyekuwa Mkurugenzi wa Idara ya Teknolojia na Habari ya Shirika la Hifadhi ya Jamii alichangia shilingi milioni moja. Masimango alifariki mwezi Julai 2013.
Tafadhali changa kwa njia zifuatazo:
Jina la Akaunti: Kijiji cha Kichalikani
Benki: National Microfinance Bank
Namba ya Akaunti: 4193300163
Tawi: Mkwakwani, Tanga.
Hata wasiopenda majina yao yachapishwe nao wanaombwa kuwasilisha hizo taarifa kwa njia hiyo ya barua pepe (majina hayatachapishwa).