Raia wa kigeni akamatwa kwa ujangili, akutwa na mikia ya tembo, kucha za simba, sare za JWTZ, silaha na risasi

RAIA wa Asia na mkazi wa Namanga jijini Dar esalam Mohamed Saqib (37) amekamatwa na jeshi la Polisi mkoani Pwani kwa tuhuma za ujangili, ku... thumbnail 1 summary
RAIA wa Asia na mkazi wa Namanga jijini Dar esalam Mohamed Saqib (37) amekamatwa na jeshi la Polisi mkoani Pwani kwa tuhuma za ujangili, kukutwa na nyara mbalimbali za Serikali pamoja na silaha tatu na risasi zaidi 50 za aina mbalimbali.

Akielezea tukio hilo jana Kamanda wa Polisi mkoani Pwani Ulrich Matei amsema raia huyo wa Asia amekamatwa majira ya saa 8 usiku jana huko Mwandege Mkuranga baada ya kutiliwa shaka na askari wa maliasili wakati akisafiri kwa gari T 448 AVM Toyoya Land Gruser kutokea wilayani Rufiji kwenda jijini Dar esalaam.

Kamanda Matei amesema baada ya kukamatwa askari walifanya upekuzi katika gari hilo na kukuta ndani yake kuna risasi 32 za silaha aina ya Rifle 270 na kipande cha nyama ya swala huku akiwa hana kibali cha umiliki wa vitu hivyo.

Amesema askari hao walimtilia shaka zaidi raia huyo na hivyo waliamua kufatilia na mazingira anayoishi raia huyo ambapo walienda hadi nyumbani kwake eneo la Block 41 Oyesterbay na kufanya upekuzi na kukutwa akiwa na nyara mbalimbali za Serikali ya wanyama mbalimbali, sare za jeshi,silaha tatu aina tofauti na risasi 51 za silaha tofauti kinyume na sheria.


Kamanda huyo ametaja vitu hivyo na idadi yake kwenya mabano kuwa ni silaha aina ya Rifle 240 na risasi zake (21),silaha aina ya Rifle 270 ,silaha aina ya aina ya short gun pump action na risasi zake (10),risasi (2) za silaha aina ya short gun two pipes,vipande (3) vya nyama aina ya nyumbu na fuvu la kichwa cha nyati  vyote akiwa hana vibali vinavyomruhusu kuvimiliki.

 Vitu vingine alivyobambwa navyo raia huyo kinyume na sheria ni Sare za JWTZ jozi (5),na suruali (2),mikia ya tembo vipande (8),kucha za simba (19),sare za askari wa TANAPA suruali(3) na koti(1),sare za askari wanyama pori suruali (1) na kikoti kimoja,kichwa cha swala,kipande cha nyama ya kongoni na fuvu la kichwa cha nyati .


Kamanda huyo ameongeza kuwa mtuhumiwa huyo anatarajiwa kufikishwa mahakamani wakati wowote upelelezi unaoendelea ukikamilika.