Mwanamitindo
wa Tanzania aishiye na kufanya shughuli zake nchini Marekani, Flaviana
Matata ataonekana kwenye tangazo la TV la vivutio vya Tanzania, ambalo
linatarajiwa kurushwa kupitia vituo vya Televisheni vikubwa duniani, CNN
na BBC.
Taarifa hiyo imetolewa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu kupitia Twitter.
“Flaviana Matata kushiriki Tangazo la vivutio vya Tanzania litakalorushwa CNN America na BBC World”
Flavianna Matata amepost tweet hiyo kwenye akaunti yake ya Instagram na kuandika:
“God’s time is the best time #ProudlyTanzanian.”