Afisaa mkuu mtendaji wa shirika
la ujasusi la Urusi, FSB, Alexander Bortnikov, amesema kuwa moto
uliozuka katika misitu na kusambaa hadi Kusini mwa bara Uropa na Balkans
msimu wa joto, ulianzishwa na kundi la Al Qaeda.
Bwana Alexander aliyasema hayo kwenye mkutano wa
kimataifa kuhusu ulinzi mjini Moscow na kuonya kuwa watu walitumia
mitandao inayomilikiwa na watu wenye siasa kali, kutuma habari kuhusu
maeneo ya kuanzishia moto huo na ambavyo wataweza kuficha ushahidi.Ingawa wanamazingira pamoja na makundi ya kutetea misitu, wanasema kuwa hakuna dalili kuwa moto huo ulianzishwa na makundi ya kigaidi.
Chanzo: BBC