KAKAKUONA AONEKANA KILWA, AUPIGA BUSU MARA MBILI MTUNGI WA MAFUTA YA GESI, WENYEJI WASEMA AMETABIRI KUWEPO KWA GESI NYINGI KILWA

 Hapo ni wenyeji wakipiga makofi na kumzunguka kwa furaha kwa neema iliyoletewa na kakakuona Usiku mlinzi aliyejawa hofu alinizi... thumbnail 1 summary
 Hapo ni wenyeji wakipiga makofi na kumzunguka kwa furaha kwa neema iliyoletewa na kakakuona


Usiku mlinzi aliyejawa hofu alinizinduwa (amsha usingizini) baada ya kuona kiumbe wa ajabu. Alikuwa ngaka (kakakuona) mwenye uzito wa kilo 32.... Hata wanasayansi wanajua machache kuhusu mnyama huyo aonekanae kwa nadra sana!
Niliwapigia simu idara ya wanyama pori waje wamchukue ili wakamhifadhi.Ukatokea mzozo na wazee wa kijiji kwamba ni lazima afanyiwe ada ya kiasili kwani ugeni wake huyo ni muhimu kuliko hata wa mgeni yoyote yule bora.Hivyo kakakuona akawekewa mkeka mpya, vikapangwa vitu muhimu vya kutabiriwa ili aweze kuabiri.
Jembe, panga, kibiriti, maji, hela, mahindi, ufuta....baada ya mimi kusema tuweke mtungi wa gesi kwani hapa kwetu gesi asilia ndio zao kuu kwetu na mimi ndio biashara yangu wazee wakasema hayo ni mambo ya kizungu lakini baadae wakakubaliana na wazo langu la kuweka mtungi wa gesi. Kama vile Ngaka alitaka kutupa huo ujumbe moja kwa moja ...paaarrrrr akikimbia hadi kwenye mtungi wa Gesi!! Akaviacha vitu vingine vyote! Wala havikukumshughulisha...amini usiamini baada ya Ngaka kuzunguka akikitupia macho kitu kimoja kimoja akaamua kuondoka na kisha kurudi kama aliesahaua kitu.... moja kwa moja mpaka kwenye mtungi wa gesi akatoa ulimi wake na kubusu mara mbili sisi tukapigwa butwaa na kupiga makofi tukiashiria neema ya gesi kwenye wilaya yetu. Hongera kilwa na Natural Gas discoveries Ngaka ametabiri hivyo.....
Habari hii nimekuta kwa mdau mmoja facebook, anatitwa Sultan A Sultan