WAREMBO REDD'S MISS TANZANIA WATEMBELEA MLIMA KILIMANJARO

Afisa Msaidizi wa Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA),Eva Mallya akitoa maelezo kwa Warembo wanaowania Taji la Redd'... thumbnail 1 summary
Afisa Msaidizi wa Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA),Eva Mallya akitoa maelezo kwa Warembo wanaowania Taji la Redd's Miss Tanzania 2012,juu ya Utaratibu wa Upandaji Upandaji wa Mlima Kilimanjaro.Warembo hawa walitembelea eneo hilo la Mwanzo wa Mlima Kilimanjaro uliopo Marangu kwa ajili ya kujifunza mambo mbali mbali ya utalii wa ndani.
Baadhi ya Warembo wanaowania taji la Redd's Miss Tanzania 2012 wakizungumza na baadhi ya wabeba Mizigo ya Watalii mbali mbali waliofika kwenye Lango kuu la Kupanda Mlima Kilimanjari,lililopo Marangu Mkoani Kilimanjaro.Warembo hawa wametembelea eneo hilo la Mwanzo wa Mlima Kilimanjaro uliopo Marangu kwa ajili ya kujifunza mambo mbali mbali ya utalii wa ndani.

Baadhi ya Warembo wakiwa Wamebeba Mabegi mithili ya Watalii wanaopanda mlima Kilimanjaro.
Baadhi ya Warembo wa Redd's Miss Tanzania wakiwa kwenye picha ya Pamoja na Baadhi ya Watalii waliokuwa wakirudi kutoka mlima Kilimanjaro.
 Warembo katika pozz
Warembo wakiwa kwenye picha ya Pamoja.
Warembo wakiondoka eneo hilo la Mwanzo wa Upandaji wa Mlima Kilimanjaro. 
Chanzo: Dar es Salaam Yetu