Penthouse Suite: Chumba cha hoteli chenye gharama kubwa duniani, Kulala kwa usiku mmoja tu ni dola 80,000

Vyumba vya suti vinaweza kuwa na gharama sana lakini kwa hali ya kawaida huwezi kuamini kama mtu anaweza kutumia bajeti kubwa katika kula... thumbnail 1 summary
Vyumba vya suti vinaweza kuwa na gharama sana lakini kwa hali ya kawaida huwezi kuamini kama mtu anaweza kutumia bajeti kubwa katika kulala usiku mmoja tu kwenye hoteli.
Suti hii yenye vyumba 12 kila chumba kikiwa na bafu, inafahamika kama the Royal Penthouse Suite ni moja ya vyumba vya Hotel President Wilson huko Geneva Uholanzi ambacho kinatajwa kuwa ndio chumba chenye gharama zaidi duniani ambapo gharama za kulala katika chumba hicho kwa usiku mmoja ni dola 80,000
Watu mashuhuri ulimwenguni waliolala katika chumba hicho ni pamoja na Rais wa zamani wa Marekani Bill Clinton, Michael Jackson, Rihanna, Richerd Branson na Bill Gates.
Chumba hicho kina makolokolo mengi, kwanza suti hiyo inaukubwa wa square feet 18,000 na inachukua ghorofa nzima ya nane ya hoteli hiyo, inavyumba vya kulala (four bedrooms), multiple living rooms, maktaba na chumba cha kulia chenye uwezo wa kubeba watu 26. Wala usijali hawa watu 26 wanalishwaje, haha.. kuna mpishi maalumu kwa gharama zako, usicheze.
Ndani ya chumba utakutana na vitu hivi, billiards, Jacuzzi, Steinway grand Piano, TV flat screen inch 103 ikiwa imewekewa sound system ya nguvu na inaonyesha vizuri picha zake yaani kama ungeinunua mwenyewe hii TV ingekugharimu dola za kimarekani 130,000.

Pamoja na hoteli hiyo kuwa na kumbi za mikutano na sehemu ya kufanyia mazoezi (fitness centers) kwa wageni wote, lakini haiwezekani kulipa dola zote hizo halafu ukaanza kutumia huduma za umma, hivyo kuna chumba maalumu cha mikutano ndani ya hiyo suti, pia kuna chumba cha pekee cha kufanyia mazoezi ambacho kiko kwenye uficho ili kuzuia kukutana na paparazzi

Security: chumba hicho kinamfumo mzuri wa ulinzi, kuna timu kabisa ya ulinzi mbali na hilo madirisha na milango yamewekewa bullet proof na kuna safe ya uhakika kuhifadhia yale mambo muhimu.