Video: Chui avamia kambi ya watalii na kuanza kunywa kahawa

Katika hali isiyo ya kawaida chui mmoja amevamia kambi ya watalii kwenye hifadhi ya Central Kalahari Game reserve huko Botswana na kufany... thumbnail 1 summary
Katika hali isiyo ya kawaida chui mmoja amevamia kambi ya watalii kwenye hifadhi ya Central Kalahari Game reserve huko Botswana na kufanya matukio ya kustaajabisha likiwemo la kunywa kahawa.
Shuhuda wa tukio hilo Attie Cilliers alisema chui huyo alifika kambini kwao muda wa usiku na kunywa maji yaliyokuwa nje na kuondoka zake, lakini ilipofika asubuhi alirudi tena na kuanza kunusa kila kitu kilichokuwa eneo hilo huku akiweka ulimi wake kwenye kahawa na kuungua.
Alikaa kwa muda kusubiri kahawa ipoe na kuendelea kunywa kabla ya kuondoka zake.
Vipande vya tukio hilo vinaonekana kwenye video ifuatayo