Warsha ya siku mbili ya mafunzo kwa wataalam wa mazingira katika utekeelezaji wa mkataba wa Stockhom yafunguliwa Arusha

 Bi Magdalena Mtengu, mkurugenzi msaidizi wa idara ya Mazingira Ofisi ya makamu wa Rais, akitoa maelezo ya utangulizi kabla ya ufunguzi wa... thumbnail 1 summary
 Bi Magdalena Mtengu, mkurugenzi msaidizi wa idara ya Mazingira Ofisi ya makamu wa Rais, akitoa maelezo ya utangulizi kabla ya ufunguzi wa warsha hiyo
Kulia mkurugenzi wa idara ya mazingira ofisi ya makamu wa rais Dkt Julius Ningu akifungua warsha ya mafunzo ya wataalamu kuhusu kemikali zinazodumu katika mazingira kwamuda mrefu..inayoanza leo mjini arusha, kushoto ni muwezashaji katika warsha hiyo profesa Jamidu katima wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Picha ya Pamoja ya washiriki wa warsha hiyo. Picha zote pamoja na habari zimeletwa kwenu  na Evelyn Mkokoi, Arusha

Nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania zinakabiliwa na changamoto ya kuongezeka kwa maeneo yaliyoathirika na kemikali zinazokaa kwa muda mrefu zaidi ardhini.

Hayo yamesemwa leo Mjini Arusha  na mkurugenzi wa idara ya mazingira kutoka ofisi ya makamu wa Rais Dkt Julias Ningu, wakati wa ufunguzi wa warsha ya siku mbili ya mafunzo ya  wataalam katika utekeelezaji wa mkataba wa Stockhom ambao Tanzania ni wanachama.

Dkt. Ningu amesema kuwa, kutokana na ongezeko la matumizi ya kemikali zinazohitajika kwa ajili ya shughuli za maendeleo. 

Changamoto hii inazidi kuongezeka siku hadi siku kutokana na upungufu wa wataalam wenye ujuzi na vitendea kazi sahihi kwa ajili ya kusimamia kemikali hizi hususan mlundikano wa madawa ya kilimo yaliyokwisha muda wake.

Dkt. Ningu aliongeza kwa kusema kuwa, changamoto nyingine za kimazingira kwa sasa ni usimamizi wa kemikali hatarishi ikiwamo kemikali zinazodumu katika mazingira kwa muda mrefu ambapo suala hili linatokana pamoja na mambo mengine ukosefu wa ujuzi wa kutosha pamoja na miongozo sahihi ya namna ya usimamizi.

“Hii inaweza kusababisha hatari ya watu kuathirika kiafya hivyo, ni jambo la msingi kujenga uwezo wa wataalam wetu katika kusimamaia na kudhibiti kemikali hizi ili kulinda afya za watu na mazingira, Alisisistiza”.

Mkataba wa Stockholm ambapo Tanzania ni mwanachama, unazitaka nchi wanachama kuweka mfumo wa kitaasisi na kisheria katika kusimamia kemikali zinazodumu katika mazingira kwa muda mrefu, pamoja na kudhibiti madhara yake kiafya na katika mazingira.