Kwa kina: Historia ya Ziwa Nyasa

Ziwa Nyasa (katika Malawi: Lake Malawi; katika Msumbiji: Niassa) ni kati ya maziwa makubwa ya Afrika ya Mashariki ikiwa na nafasi ya tatu... thumbnail 1 summary
Ziwa Nyasa (katika Malawi: Lake Malawi; katika Msumbiji: Niassa) ni kati ya maziwa makubwa ya Afrika ya Mashariki ikiwa na nafasi ya tatu baada ya Viktoria Nyanza na Ziwa Tanganyika.

Lina urefu wa 560 km na upana wa 50-80 km. Vilindi vyake vinaelekea hadi mita 704 chini ya uwiano wa maji yake.
Ziwa Nyasa linapatikana kati ya nchi za Malawi, Msumbiji na Tanzania.
 Mwonekano wa Jiwe la kihistoria kwa ubavuni linalojulikana kwa jina Pomonda lililopo Ziwa Nyasa lililotumiwa kujificha na wananchi wakati wa Vita vya Dunia.

 Jiwe la POMONDA likionekana kwa nje katika Ziwa Nyasa eneo la Liuli.
 Kivutio kimoja wapo katika Mwambao wa Ziwa Nyasa katika eneo jirani na Jiwe la Pomonda ni Machweo ya Jua (SUNSITE)kama yanavyoonekana pichani kwa mbali
 Jiwe la POMONDA lililopo katika Ziwa Nyasa hapo ni nje ya Pango ambalo kwa ndani lina uwezo wa kuhifadhi watu 250 kwa wakati mmoja hapo ni namna maji kupwa yanavyoonekana pembeni mwa jiwe hilo.
 Ufukwe wa Ziwa Nyasa namna unavyoonekana pichani na kuvutia kwa Madhari ambapo shughuli za kiuchumi kwa Wananchi wa Ziwa Nyasa huzifanya eneo la Mwambao wa Ziwa Nyasa au kuvuka Nchi jirani ya Malawi ambayo imetenganishwa na Ziwa Nyasa.
 Washiriki wa Mdahalo wa Mabadiliko ya HAli ya Hewa uliofanyika Liuli Wilayani Nyasa kwa Ufadhili wa Foundation for Civil Society wakionyesha Jiwe la POMONDA linalovutia watalii mbalimbali wanaokuja kutembelea Ziwa Nyasa.
 Hapo ni Meli ya MV Songea ambayo hutumika kusafirisha Abiria na Bidhaa kutoka Tanzania kuelekea Malawi kupitia Ziwa Nyasa ikiwa imetia Nanga Liuli Ziwa Nyasa

 Kutoka eneo la Ufukwe mpaka kulifikia Pango hili la Pomonda kuna umbali wa kilometa moja na robo. Pango hili la Pomonda limezungukwa na Miti ya Asili ambayo uneune wake hauzidi robo mita na umri wa miti hiyo yapata miaka 100,pango hili la Pomonda pia limezungukwa na Mawe yenye umbo la Mafiga Matatu kuzunguka eneo hilo mpaka kulimaliza unachukua muda wa saa . Hapo Mwandishi wa Habari Adam Nindi baada ya Kuzunguka katika kulifikia pango hilo inaonyesha jinsi gani alivyochoka akiwa amelala chini. 
 Taarifa zilizotolewa na Wazee waishio katika eneo la Mwambao wa Ziwa nyasa wamesema kipimo cha ujazo wa Maji ya Ziwa Nyasa kujua yanapungua au yanaongezeka ni alama hizo zinazoonekana mistari mieupe na rangi nyeusi kuwa ziwa limepungua maji kwa kiasi kikubwa ambapo awali yalifikia katika mistari inayoonekana kwenye jiwe hilo
ewa 


Kusini mwa ziwa unatoka Mto Shire unaopeleka maji kwenye Mto Zambezi na hatimaye Bahari Hindi.
Kijiolojia ziwa ni sehemu ya Bonde la Ufa la Afrika ya Mashariki.

Eneo la ziwa ni 29,600 km². Sehemu kubwa ni eneo la Malawi, robo ya kusini-mashariki ni eneo la Msumbiji, robo ya kaskazini-mashariki ni eneo la Tanzania. Lakini kuna ugomvi kati ya Malawi na Tanzania kuhusu mipaka. Malawi imedai ya kwamba maji yote hadi ufukoni upande wa Tanzania ni sehemu ya eneo lake la kitaifa. Tanzania imedai ya kwamba mpaka uwepo katikati kufuatana na uzoefu wa kimataifa.

Sababu ya mzozo ni utaratibu wa kikoloni. Wakati wa Afrika ya Mashariki ya Kijerumani palikuwa na mpaka wa kimataifa kaskazini mwa ziwa. Baada ya 1919 Uingereza ilitawala Tanganyika pamoja na Malawi (Nyasaland). Kwa kusudi la kurahisisha utawala mambo yote yaliyohusu ziwa yaliwekwa chini ya serikali ya kikoloni ya Nyasaland. Baada ya uhuru Malawi ilijaribu kutumia uzoefu huo kama haki yake ya kitaifa. Polisi yake ilijaribu kutawala wavuvi na feri za Tanzania ziwani. Mzozo huu ulisababisha risasi kufyatuliwa baada ya uhuru. Hadi leo hakuna mapatano rasmi lakini nchi zote mbili zinaendelea bila kutumia nguvu. Hali halisi Malawi imeheshimu dai la Tanzania halikusumbua tena wavuvu au feri za jirani ndani ya robo ya kaskazini-mashariki ya ziwa.
Ziwa Nyasa linajulikana kuwa na aina nyingi za samaki (zaidi ya 1500). Aina chache tu zinavuliwa kama chakula lakini aina mbalimbali zinakamatwa na kuuzwa nje ya Afrika kwa wapenzi wa samaki zenye rangi.