Picha: Mjasiriamali ajenga hoteli ya miti yenye gorofa

  NA MUTAYOBA ARBOGAST,Harakatinews Missenyi KIJANA mmoja Frank Anthony Rumanyika(30)  pichani juu  wa kijiji cha Bukabuye kata ya Bw... thumbnail 1 summary
 

NA MUTAYOBA ARBOGAST,Harakatinews Missenyi

KIJANA mmoja Frank Anthony Rumanyika(30)  pichani juu  wa kijiji cha Bukabuye kata
ya Bwanjai ni mjasiriamali mbunifu.

Mwezi Machi 2013 aliamua kuchepuka toka ndani ya kijiji chao na akaanzisha makao ya kibiashara karibu na makutano ya barabara ya  Kanyigo-Bukoba na Kanyigo-Mugana,

Akajenga kijumba cha kuvutia cha miti na nyasi kwa mtindo wa ghorofa na hapo pakashika jina kwa KAGHOROFA KA KAMAGUSHU kwa kuwa eneo lile linaitwa Kamagushu.Anasema alianza na mtaji wa sh 80,000/ tasilimu pamoja na ule mtaji ambao hakuweza kuuthamanisha fedha wa unaoitwa mtaji wa masikini ni nguvu zake mwenyewe.


Biashara ilianza kumnyokea lakini watu wabaya wakamtia hasara kubwa walipochoma moto vijumba vyake vya biashara,usiku wa  29 Januari mwaka huu.Palibaki majivu tu! Anasema waliochoma walikamatwa ila aliyewatuma alitoroka na kuwa kesi ipo mahakamani-wivu wa kibiashara.

Hakukata tama.ameanza tena kupajenga na  anasema atajitahidi kuimarisha ulinzi na anakataa kabisa tetesi kwamba labda alikuwa akikaribisha wake na waume za watu 'kukutana'

Anasema pamoja na juhudi zake tatizo ni kutokuwa na mtaji wa biashara hivyo anaomba wenye mapenzi mema wamsaidie kupitia namba yake ya  simu   0786671160