Kamati Tendaji ya Umoja wa Wabunge
wa Uhifadhi na Matumizi Endelevu ya Wanyamapori iliyoketi mjini Dodoma chini ya
Mwenyekiti wake, Riziki Saidi Lulida, kuchambua sheria ya uhifadhi ya
wanyamapori ya mwaka 2009 inapenda kuufahamisha umma kuwa imebaini Tanzania
inapaswa kutumia njia tatu ambazo zitasaidia kudhibiti ujangili. Njia hizo ni
hizi zifuatazo.
1 - Taifa linapaswa kudhibiti
masoko yanayotumika kwa biashara haramu ya nyara za Taifa.
2- Taifa linapaswa kudhibiti njia
za kusafirisha nyara za Taifa.
3- Taifa linapaswa kudhibiti
uwindaji haramu katika hifadhi na ili kudhibiti ujangili ni lazima tuwe na “comprehensive
doctrine, strategy, tactics.”
Katika uchambuzi wa tatizo la
msingi la ujangili hapa nchini, kamati ilibaini kuwa ujangili ni sawa na mchezo
wa PAKA na PANYA. “We need the right cats.” Ili kuondoa tatizo la ujangili,
taifa linahitaji “comprehensive, intelligent and pragmatic doctrine that
addresses all the problems and offers objective and inexpensive solutions,
preferably using local resources and personnel.
Hata hivyo, ili kufikia mkakati wa
kukabiliana na tatizo la ujangili nchini kamati ilibaini kuwa kama taifa
tunahitaji kuainisha maeneo ambayo tunaweza kuwaona au kuwapata majangili na
ili kufanikisha hili tunahitaji, Pro-active Investigators” (Expert
Investigators are needed.)
Investigations
can be both pro-active are reactive.
Proactive, should go hand in hand
to benefit people ambao ni muhimu katika harakati za kulinda wanyamapori
(Wananchi ndiyo walengwa katika mkakati huu.)
The community has to be engaged to
assist efforts and most if at all possible benefit from the tourism and other
revenue and prestige earnings and job creating activities.
Iwapo hili litafanyika, Wananchi
watashiriki kuonyesha maeneo wanayojificha majangili na hii ni kwa sababu
majangili huhitaji msaada wa Wananchi kupata silaha, chakula, maji na zana
nyingine za kufanikisha ujangili.
Pia hutumia Wananchi wanaoishi
maeneo yanayozunguka hifadhi kubeba nyara mbalimbali za Taifa (pembe, ngozi,
kucha, n.k. hivyo Wananchi ni chanzo muhimu cha kupata taarifa mahsusi za
mienendo ya majangili ndani na nje ya maeneo ya hifadhi. Hivyo, wachunguzi au
scouts, rangers waliofunzwa mambo ya uchunguzi wanaweza kukusanya taarifa
kutoka kwa Wananchi kuhusu “Previous Poaching Activities.”
Tatizo jingine linalohitaji
kushughulikiwa ni namna ya kuwasaka majangili baada ya kupata taarifa ya
mienendo yao, maeneo wanayoyatumia au kujificha. Hili linahitaji ufuatiliaji
ambao husaidia kuelewa mapito ya majangili sawa na namna wafugaji wanavyoweza
kuelewa mienendo ya wanyama wakali.
Kamati inaamini kuwa bila shaka
ziko droves ambazo zinaweza kuruka chini kwa chini na kufanya kazi nzuri lakini
gharama yake ni kubwa sana hivyo ni jambo zuri tutumie wananchi kupambana na
ujangili.
Tatizo jingine lililooneaka ni
namna ya kuwakamata majangili. Ni vigumu na ni hatari kwa anayefuatilia
mwenendo wa jangili anapomuona kumkamata mara moja kwa sababu jangili anaweza
kujihami hivyo kuweka mazingira magumu ya kumkamata.
WAJIBU WA
WANANCHI
Kamati inapenda kuufahamisha umme
wa Watanzania kuwa Ibara ya 4 ya Sheria hii inatamka kuwa wanyamapori wote
nchini Tanzania ni mali ya Umma na watakuwa chini ya dhamana ya Rais kwa niaba
ya Watanzania.
Pili, Ibara 4 (2 – 6) inaelekeza
utaratibu kwa mtu au watu binafsi kumiliki mnyama au wanyama.
Na inawakumbusha wananchi wote kuwa
malengo makuu ya Sheria ya Uhifadhi wa Wanyamapori ni kuendeleza rasilimali za
wanyamapori kwa maendeleo ya uchumi na ustawi wa maisha ya Watanzania na
kutunza sekta ya utalii kwa vizazi vya sasa na vijavyo.
Ibara 15 (1) inakataza mtu yeyote
asiyehusika kuingia katika maeneo ya uhifadhi isipokuwa wasafiri wanaopita kwa
usafiri wa magari kwenye mbuga au boti kwenye maziwa n.k na Ibara ya 15
(2) inatoa adhabu kwa anayevunja katazo 15
(1) kama anapatikana na hatia atatozwa faini isiyopungua Tshs.100,000 na
isiyozidi Tshs. 500,000.
Aidha Ibara 17 (1) inakataza mtu
kumiliki silaha, upinde, mishale na aina nyingine ya silaha ndani ya pori la
akiba na Ibara ya 17 (2) inatoa adhabu kwa anayevunja maelekezo ya Ibara 17 (1)
ambayo haitazidi Tshs 200,000 au kifungo cha miaka mitatu jela au vyote.
Pia Ibara 20 (1) inakataza
mtu kufanya shughuli yeyote katika maeneo ya hifadhi ikiwemo kuchimba au
kukusanya mchanga, madini n.k na Ibara 26 (1) fasili (1) inakataza mtu yoyote
kufanya shughuli za uwindaji isipokuwa kwa ruhusa maalumu.
Watanzania wanapaswa kukumbuka kuwa
wakati wa uhuru, Tanzania ilifanikiwa sana katika uhifadhi wa wanyamapori kwa
sababu ya sera thabiti zilizotungwa chini ya uongozi wa Baba wa Taifa, Mwalimu
Julius Nyerere.
Katika moja ya matamko yake,
Mwalimu Nyerere alipata kueleza kwa lugha ya kiingereza kuwa, “The survival
of our wildlife is a matter of grave concern to all of us in Africa. These wild
creatures amid wild places they inhabit are not only important as a source of
wonder and inspiration but are an integrate part of our natural resources and
of our future livelihoods and well being”.
Na aliwahi pia kusema ni jukumu la
Watanzania kuhakikisha kwamba rasilimali za wanyamapori zinanufaisha Watanzania
na watoto wa wajukuu wao. Hivyo, jukumu la kulinda wanyamapori ni la Watanzania
wenyewe siyo Askari Pori “Game Rangers au Police na
madhara yatokanayo na uharibifu wa rasilimali ya wanyamapori haitaathiri
Tanzania peke yake bali Bara lote la Afrika na Dunia kwa ujumla wake.
Umma wa watanzania unapaswa
kufahamu kuwa matatizo makuu yanayokabili uhifadhi hapa nchini ni kuwepo kwa
sera dhaifu inayoshindwa kuainisha majukumu ya Wananchi wanaoishi maeneo
yanayozunguka hifadhi na Mapori ya Akiba.
Na pamoja na mambo mengine mengi ya
msingi, ufinyu wa bajeti na watendaji unasababisha Serikali kushindwa
kuwashirikisha Wananchi wanaoishi Vijijini kushiriki masuala ya uhifadhi.
Kamati pia imebaini upungufu katika
sera ya Uhifadhi wa Wanyamapori. Kwamba Sera imeshindwa kuonyesha namna
watakavyoshirikishwa Wananchi wanaoishi maeneo yenye hifadhi na yanayozunguka
Mapori ya Akiba watakavyoshirikishwa katika majukumu ya uhifadhi.
Sambamba na hilo, pia Wananchi
hawajapewa elimu sahihi inayoonesha umuhimu wa wanyamapori kwa uchumi wao na
Taifa na Sera imeshindwa kuonyesha mbinu na mikakati au mipango ya kuondoa au
kupunguza ugomvi kati ya wafugaji, wakulima na Hifadhi za Taifa.
Riziki Said Lulida (MB)
MWENYEKITI
TANZANIA
PARLIAMENTARY GROUP ON SUSTAINABLE NATURAL RESOURCES CONSERVATION AND
UTILIZATION (TPGSNRCU)