February 9 mwaka huu, gazeti la Daily Mail la Uingereza liliandikia kuwa “Tanzania inaua tembo zaidi ya 11,000 kwa mwaka kwaajili ya biashara ya pembe za ndovu na Rais wake amefumbia macho’.
Lilidai kuwa theluthi ya pembe zote za ndovu zinazokamatwa barani Asia
hupitia Tanzania na kila siku tembo 30 huuliwa ambao ni sawa na tembo
11,000 kila mwaka. Habari hiyo iliipa Tanzania sifa mbaya hali ambayo
imewasukuma Mrishi Mpoto na Peter Msechu kutumia sauti zao kukemea
mauaji tembo na vifaru.
Mrisho Mpoto na Peter Msechu wakiongea na waandishi wa habari
Wasanii
hao waliokuwa na mkutano na waandishi wa habari leo, wameungana
kuanzisha kampeni yao ya kupambana na ujangili dhidi ya tembo na vifaru.
“Tumeachia
wimbo mpya na video yake unaoitwa DENI LA HISANI pia tumerelease rasmi
tshrt zetu zinazoitwa USINIUE NITUNZE… Tunawaomba wote tuungane kwa
pamoja tupinge mauaji dhidi ya wanyama wasio na hatia,” ameandika Peter
Msechu kwenye Instagram.