Msanii kulala ndani ya tumbo la Dubu

Msanii mmoja nchini Ufaransa anajiandaa kulala ndani ya tumbo la Dubu ... thumbnail 1 summary
Msanii mmoja nchini Ufaransa anajiandaa kulala ndani ya tumbo la Dubu wake aliyewindwa na kuhifadhiwa katika makavazi ya wanyamapori mjini Paris.

Uamuzi wake huu umetajwa kama kuchagua kati ya maisha ya binadamu na wanyama.
Msanii huyo mfaransa anaanza maonyesho yake ya kiusanii ambayo yametajwa kuwa ya kipekee na ambayo yatashuhudia akilala ndani ya mnyama huyo kwa siku 13.
Abraham Poincheval aliyezaliwa mwaka 1972 kwa mara ya kwanza alifanya maonyesho hayo yanayojulikana kama -kuishi ndani ya ngozi ya Dubu- katika kituo cha maeonyeso ya usanii mjini Digne mwaka jana.
Sasa anajiandaa kurejelea onyesho hilo katika makavazi mjini Paris ambako atasalia ndani ya tumbo la Dubu huyo ambaye ni mnyama halisi isipokuwa tu amekaushwa na kuhifadhiwa katika makavazi hiyo.
Abraham Poincheval akichunguza ndani ya Dubu wake katika makavazi ya wanyama waliowindwa na kuhifadhiwa.
Poincheval aliwahi kuishi ndani ya shimo chini ya maktaba mjini Marseilles Oktoba mwaka 2012.
Inaarifiwa mwanaume huyo ni mjuzi wa maonyesho ya usanii yenye kutumia mbinu hatari.
Poincheval atakula, kulala na hata kwenda haja akiwa ndani ya tumbo la Dubu huyo, huku akinaswa na kamera mbili.
Abraham Poincheval akipanda ndani ya Dubu wake kabla ya kuonyesha atakavyojifungia ndani
Duru zinasema kuwa kilichompa Poincheval motisha ya kuishi ndani ya mzoga wa mnyama huyo, ni mizoga ya wanyamapori aliyokuwa anakutana nayo mara kwa mara nchini Ufaransa.
dubu