Chanzo: Bongo5
Wamiliki
wa msululu wa supermarket kubwa za Kenya, Nakumatt, watatakiwa kusubiri
hadi katikati ya mwaka huu kabla ya kununua supermarket tatu za kampuni
ya Shoprite ya Afrika Kusini zilizopo nchini.
Manunuzi
hayo yalitakiwa kufanyika mwezi huu wa nne lakini sasa yatafanyika
baada ya miezi mitatu kwa mujibu wa tume ya ushindani Tanzania, FCC.
“Hatuna uhakika lini tutachukua maduka hayo kwakuwa tumeambiwa na tume
ya ushindani ya Tanzania kungoja kwa miezi mitatu mingine,” alisema
Thiagarajan Ramamurthy, Head of Strategy and Operations wa Nakumatt.
Sababu za kuchelewa huko hazijatajwa.
Supermarket
hizo zitauzwa kwa gharama ya dola milioni 40.45. Nakumatt imeahidi
kuwaajiri wafanyakazi wa Shoprite pale itakapozinunua ili kupunguza
gharama ya kuajiri wafanyakazi wapya. Kampuni hiyo ya Afrika Kusini
inaondoka Tanzania baada ya kuonywa kuacha kuchukua bidhaa kutoka Afrika
Kusini na kutopromote zile za Tanzania.
Kwa
upande wake Nakumatt imepanga kuwapa kipaumbele wazalishaji wa bidhaa
wa Tanzania na wale wa Kenya waliopo Tanzania. Hatua hiyo ya
kuchelewashwa kwa manunuzi hayo kunaiathiri Nakumatt ambayo ilikuwa
imejipanga kuanza biashara mwezi huu.