Mkutano wa Mabadiliko ya Tabianchi wafanyika jijini Dar es Salaam

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Profesa Rwekaza Mukandara akifungua mkutano wa mabadiliko ya tabianchi unaofanyika katika... thumbnail 1 summary
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Profesa Rwekaza Mukandara akifungua mkutano wa mabadiliko ya tabianchi unaofanyika katika hoteli ya Kunduchi nje kidogo ya jiji la Dar Es salaam ukiwashirikisha watafiti na wanamazingira kutoka nchi mbalimbali za Afrika ikiwemo Tanzania.
Mkurugenzi wa kituo cha mafunzo ya mabadiliko ya tabianchi cha chuo kikuu cha Dar Es Salaam Profesa Pius Yanda akiwasilisha mada katika mkutano huo.
Profesa Mukandara akijadiliana na wataalam wanaoshiriki kwenye mkutano huo muda mfupi baada ya ufunguzi wa mkutano huo unaofanyika Kunduchi nje kidogo ya jiji la Dar es salaam.
Wataalam wa mazingira na watafiti kutoka vyuo vikuu mbalimbali kikiwemo cho kikuu cha Dar es salaam na wadau wengine wa mazingira wanaohudhuria mkutano huo wa mabadiliko ya tabianchi katika picha ya pamoja na mgeni rasmi Profesa Rwekaza Mukandara muda mfupi baada ya ufunguzi wa mkutano huo.Picha zote na Vedasto Msungu.