WAZIRI AKABIDHIWA NDEGE ITAKAYOSAIDIA HARAKATI ZA KUKOMESHA MASUALA YA UUAJI WANYAMA PORI NA UJANGILI

 Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni inayojihusisha na ushauri na mawasiliano ya masoko ya East African Unique, Rodgers Mbaga (kulia) akizungu... thumbnail 1 summary
 Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni inayojihusisha na ushauri na mawasiliano ya masoko ya East African Unique, Rodgers Mbaga (kulia) akizungumza na waandishi wa habari jijni Dar es Salaam kuhusu maonyesho ya kukuza uwekezaji (TIPEC) nchini. Kushoto ni Meneja Mradi huo Tony Obura.
 Waziri wa Maliasili na Utalii Lazari Nyalandu (kushoto) akikabidhiwa ndege aina ya Micro Light Nyinja, 5H-HEL, na Mwenyekiti wa Kampuni ya Utalii ya Tanganyika Wildlife Safari, Eric Pasanisi, werngine ni Askari wa kikosi cha wanyamapori walio hudhuria makabidhiano hayo.
 Waziri wa Maliasili na Utalii Lazari Nyalandu (kushoto) akikabidhiwa ndege aina ya Micro Light Nyinja, 5H-HEL, na Mwenyekiti wa Kampuni ya Utalii ya Tanganyika Wildlife Safari, Eric Pasanisi, werngine ni Askari wa kikosi cha wanyamapori walio hudhuria makabidhiano hayo.
Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu akiwa na Rubani wa ndege aina ya Micro Light Nyinja, muda mfupi kabla ya kukabidhiwa ndege hiyo. Ndege hiyo ambayo imenunuliwa na kampuni ya Tanganyika Wildlife Safari ilikabidhwa kwa Waziri Nyalandu kwaajili ya kufuatilia majangili kwenye hifadhi za taifa.

Na Mwandishi Wetu

WAZIRI wa Maliasili na Utalii Lazaro, Nyalandu amepokea ndege aina ya Micro Light Nyinja 5H-HEL, kutoka kwa kampuni inayojihusisha na masuala ya utalii ya Tanganyika Wildlife Safari itakayosaidia harakati za kukomesha masuala ya uuaji wanyama pori na ujangili.

Akipokea ndege hiyo jijini Dar es Salaam Nyalandu aliasema ndege hiyo ni mpya kabisa na ya usalama wa hali ya juu kutokana na muundop wake kuwa wakisasa zaidi.

Hii ndege ni salama zaidi kwasababu yenyewe imejengwa na parachuti yake endapo kunatokea chochote wakati ikiwa angani inafunguwa parachuti ambayo itaisaidia yenyewe pamoja na watu waliomo hivyo ni ya uhakika zaidi. alisema Nyalandu.

Nae Mwenyekiti wa kampuni iliyotoa ndege hiyo ya Tanganyika Wildlife Safari, Eric Pasanisi, alisema ndege hiyo inathamani ya Dola laki mbili na ishirini elfu ($220,000), na kueleza sifa mbalimbali za ndege hiyo.

"Ndege hii ni ndege yenye spidi ndogo zaidi kuliko ndege yeyote, kwani mwendo wa ndege hii ni karibu sawa na mwendo wa gari tu, kutokana na hali hiyo itakuwa rahisi zaidi kuwabaini majangili walipo kwavili mwendo wake ni mdogo." alifafanua Eric.

Aidha Eric alisema mbali na hilo ndege hiyo pia inatumia petroli hivyo ni ya gharama nafuu zaidi kuliko ndege za kawaida.