Pinda kuzindua Siku ya Mizinga ya Nyuki

na Asha Bani WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika siku ya taifa ya kutundika mizinga ya nyuki ambayo itazin... thumbnail 1 summary



na Asha Bani
WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika siku ya taifa ya kutundika mizinga ya nyuki ambayo itazinduliwa kwa mara ya kwanza Machi 4 mkoani Singida.
Msemaji Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, George Matiko, alisema jana kuwa siku hiyo itafanyika katika Hifadhi ya Aghondi, iliyoko wilayani Manyoni.
Alisema lengo la siku hiyo ambayo itakuwa inaadhimishwa kila mwaka ni kuwahamasisha wananchi kushiriki kwa wingi katika shughuli za ufugaji nyuki kwa kutumia mbinu za kisasa.
“Wizara itatumia siku hiyo kuonyesha kwa vitendo shughuli za ufugaji nyuki, kama vile kuandaa maeneo mapya ya ufugaji nyuki, kutayarisha mizinga ya nyuki, kutafuta makundi ya nyuki kwa ajili ya kuhamishia kwenye mizinga ya kisasa na kutayarisha vifaa vya ufugaji nyuki,” alisema Matiko.
Aidha alisema katika maadhimisho hayo itatolewa elimu kuhusu kalenda ya mwaka ya ufugaji nyuki nchini na umuhimu wa kuizingatia wakati wa kufanya shughuli za ufugaji nyuki katika maeneo mbalimbali husika.

Chanzo: Tanzania Daima


Una taarifa, picha za usafiri wa anga, mazingira, maliasili na utalii? tutumie kupitia kingkahindi@gmail.com