UELEWA MDOGO WAKWAMISHA BIASHARA YA UTALII SERENGETI

UELEWA mdogo wa jamii ni chanzo cha biashara duni ya Utalii wilaya ya Serengeti Mkoani Mara ambayo inazungukwa na asilimia 70 ya eneo la ... thumbnail 1 summary
UELEWA mdogo wa jamii ni chanzo cha biashara duni ya Utalii wilaya ya
Serengeti Mkoani Mara ambayo inazungukwa na asilimia 70 ya eneo la
hifadhi na mapori ya akiba.
 
Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya hiyo John Ng’oina amesema hayo
wakati anafungua semina ya wadau kwenye ukumbi wa Maktaba mjini Mugumu
kujadili namna ya kuinua biashara hiyo,na kuwataka wazazi kuwasomesha
watoto wao,kwa kuwa elimu ndiyo itafanya mapinduzi ya kimitizamo.
 
Mshauri wa Matumizi bora ya Maliasili wilaya hiyo kupitia Mpango wa
shirika la Maendeleo la Kijermani Bw,Bennie Bloemberg amesema fursa
hiyo inapaswa kujibu changamoto za jamii kiuchumi kama itatumiwa
vizuri.
 
Amesema kupitia mpango huo wanataraji kuunda bodi ya Utalii ya
wilaya,kuandaa fursa zilizomo na kuzitangaza ili kuwawezesha wageni
kuja kuwekeza,na kufungua fursa kwa wananchi Ili waweze kunufaika
kiuchumi.
 
Hata hivyo baadhi ya washiriki wameomba serikali kuhakikisha barabara
ya lami inajengwa ambayo itasaidia kufungua fursa nyingi za kiuchumi
na kuwawezesha watu kuleta bidhaa kwa gharama nafuu.