WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII MHE. LAZARO NYALANDU AZINDUA TOVUTI LA KONGAMANO LA UFUGAJI NYUKI DUNIANI

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Lazaro Nyalandu wakati akizindua Tovuti ya ufugaji nyuki Dunianikwenye ukumbi wa kimataifa wa mikutan... thumbnail 1 summary
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Lazaro Nyalandu wakati akizindua Tovuti ya ufugaji nyuki Dunianikwenye ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Mwalimu Nyerere uliopo jjini Dar es Salaam.


Waziri wa Maliasili na Utalli, Mhe . Lazaro Nyalandu amezindua tovuti ya kongamano la Ufugaji nyuki duniani kwa lengo la kuboresha ufugaji nyuki na kupanua wigo kwa wananchi wengi kuweza kushirikiki katika ufugaji huo.
Uzinduzi wa tovuti hiyo umefanyika kwenye ukumbi wa Kimataifa wa mikutano wa Mwalimu Nyerere uliopo jijini Dar es Salaam. .
Mhe. Nyalandu amesema kuwa Tovuti hiyo ni jukwaa muhimu sana katika kuhamasisha wananchi kuitikia wito wa kujiunga kwa pamoja kuzalisha asali yenye ubora wa kimataifa pamoja na kulinda mazingira ambayo ndio muhimili mkuu wa ufugaji wa nyuki nchini.
Aidha , Mhe. Nyalandu alisema kuwa Tovuti hiyo itakuwa ni ya kudumu ili kuwazesha watanzania kuweza kujifunza masuala mengi ya ufugaji nyuki.
Alisistiza kuwa Tanzania inajivunia sana kwa kupiga hatua kubwa katika suala la ufugaji nyuki kwa kuwa ufugaji wa nyuki umepata uzito na kupewa kipaumbele kwa muda mfupi sana na hivi sasa matokeo yake yanaonekana.

Aliongeza kuwa Tanzania ni nchi ya pili Afrika kwa uzalishaji wa asali na nta hivyo kupitia kongamano linalotarajiwa kufanyika jijini Arusha tarehe 11 hadi 16 mwezi novemba litawasaidia sana wafugaji nyuki kuongeza uzalilishaji wa asali bora na kuifanya Tanzania kuwa soko kuu la asali na mazao ya asali duniani.

‘’Kongamano hili ni muhimu sana kwa Wafugaji nyuki wadogo na wakubwa pamoja na wajasilimali wa mazao ya nyuki kwani litawapa nafasi kubwa sana ya kubadilishana uzoefu na jinsi ya kuboresha ufugaji wa nyuki ikiwa na ni pamoja kujua njia bora na za kisasa za ufugaji nyuki’’
Mhe. Nyalandu alisema kwamba kongamano hili litawapa nafasi adimu watanzania kuweza kujitathmini katika uzalishaji wa nyuki wa kisasa ikiwa ni nyenzo muhimu sana ya kuweza kuzuia majangili kwani watu wengi sana wataweza kuelimika na kuilinda mazingira kwa kuzuia ukataji miti ovyo.
Kongamanp hili liwakuwatanisha wataalam wa ndani na nje wa masuala ya nyuki wakiwemo wa wafanyabiashara , wanasheria wanaharakati, wanamazingira , wanasayansi na wanafunzi wanaosomea masuala ya nyuki kujadili kwa mapana katika kuboresha tasnia ya ufugaji nyuki.
Aidha, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Maimuna Tarishi ametoa wito kwa Watanzania wote kushiriki kikamilifu katika kongamano hilo litakalofanyika mwezi wa kumi la ufugaji nyuki duniani kwa kuwa kutakuwa na wakalimani watakaowezesha kila mtanzania kujua kitachoongelewa kwenye kongamano hilo pamoja na kuchangia mawazo yake jinsi ya kuboresha ufugaji nyuki nchini.