unayajua maradhi yanayosababishwa na matango? ni hatari

Matango ni aina ya matunda ambayo yana vitamini nyingi. © REUTERS Watalaam wa afya nch... thumbnail 1 summary

Matango ni aina ya matunda ambayo yana vitamini nyingi.
Matango ni aina ya matunda ambayo yana vitamini nyingi.
© REUTERS

Watalaam wa afya nchini Ujerumani wanasema kuwa maradhi yanayosababishwa na matango ni bakteria wapya, na wanaweza kuathiri maini na damu ya mtumiaji.

Backteria hao ambao walizuka huko Ujerumani na Sweden tangu mwaka jana na  kusababisha vifo vya takriban watu 18 na zaidi ya watu 1500 wakiwa wameathiriwa na backteria hao baada ya kula matango hayo.

Waatam wa kiafya kutoka Shirika la Afya Duniani WHO wanasema kuwa hali hiyo haijawahi kushuhudiwa, huku wanasayansi kutoka China wakidai kuwa bakteria hao ni hatari sana na wana sumu ambayo pia inaweza kusambazwa kwa haraka.


Bakteria hao wamesababisha idadi kubwa ya watu kuharisha nchini Ujerumani na wataalam wa kiafya wameonya wasafiri wanaoelekea Ujerumani, kutokula matango hayo kwani yanaweza hatarisha usalama wa maisha yao.