Ili
utalii uweze kuendeshwa katika mkoa huu kunahitajika mambo kadhaa kama, Miundo
mbinu ya mawasiliano, mahoteli ya kisasa, usafiri wa anga wan chi kavu na
bahari na wakazi wake kuwa tayari kuwapokea watalii na kufanya kazi vizuri
katika maeneo ya huduma za kitalii. Baadhi ya huduma hizo Serikali kuu imetoa
kwa mfano ujenzi wa daraja la Mkapa na ujenzi wa barabara ya Mingoyo Lindi
Kibiti ambao unaendelea.
Mahoteli na nyumba za kulala wageni
Miji
ya mkoa huu haina hoteli za kutosha na za kisasa vivutio vya Utalii. Lindi
mjini hakuna Hoteli ya Kitali. Zilizopo hazipo katika “Standard” ya juu. Hazina
uchaguzi wa chakula maji yake ya kuchota nay a shida umeme nao sio wakuaminika.
Hali hii pia imeikumba wilaya ya Liwale. Kilwa kuna hoteli chache zinazotoa
huduma kwa Watalii.
Usafiri
Hakuna
usafiri wa kuamnika toka Dar es Salaam hadi Kilwa, Lindi na Liwale. Safari
tours zinahitajika. Panatakiwa pia usafiri wa boti toka Kilwa masoko kwenda
Kilwa Kisiwani halikadhalika wa kwenda songo Mnara.
Usafiri wa anga na viwanja vya ndege
Kiwanja
cha ndege cha Kikwetu cha Lindi mjini ni kizuri na kinatumika hata kwa ndege
kubwa. Kinachotakiwa ni huduma ya usafiri toka uwanjani kuja mjini Lindi.
Uwanja
wa Kilwa ni mdogo tena upo katikati ya mji. Uwanja mpya unatakiwa ujengwe nje
kidogo ya mji (Maoni ya mwandishi).
Vivutio vya mafuta.
Kunahitajika
vituo vingi vya mafuta mjini Lindi, Nangurukuru, Kilwa na Liwale. Pia ni busara
kuwa na kituo cha mafuta kati ya Nangurukuru na Liwale, ingefaa Njinjo
kungejengwa kituo hicho. Vituo vichache vya mafuta vilivyopo vinaendeshwa na
matajiri wenye mitaji midogo na mara kwa mara huishiwa mafuta.