IFAHAMU HIFADHI YA TAIFA YA KISIWA CHA RUBONDO, MOJA YA KIVUTIO CHA UTALII MKOANI MWANZA.

Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Rubondo inapatikana Kusini Magharibi mwa Ziwa Viktoria na umbali wa kilometa 150 kutoka Jiji la Mwanza. Hif... thumbnail 1 summary
Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Rubondo inapatikana Kusini Magharibi mwa Ziwa Viktoria na umbali wa kilometa 150 kutoka Jiji la Mwanza.

Hifadhi hii ya kipekee ina utajiri mkubwa wa misitu ya asili ambayo inatoa makazi kwa wanyamapori wa aina mbalimbali wakiwemo Tembo, Twiga, Mbega mweusi na mweupe, Suni na ndege mbalimbali. Pia ni moja ya maeneo muhimu ya mazalia ya ndege wahamao pamoja na jamii ya samaki ya Tilapia.

Kisiwa hiki cha Rubondo kinatoa shughuli tofauti za utalii ikiwemo uvuvi wa burudani (sport fishing) ambayo ni moja shughuli kuu ya Hifadi hii. Aina nyingine ya utalii ni utalii wa kutumia boti ambapo watalii wanapata fursa ya kutembelea maeneo ya fukwe za Ziwa Viktoria na kujionea makazi ya ndege na mamba kutumia boti. Pia Hifadhi inafanya utalii wa kutembea kwa miguu kwa muda wa masaa 2 hadi 7.


Kipindi kizuri cha kutembelea Hifadhi hii ni wakati wa kiangazi Juni hadi Septemba na kipindi cha masika kati ya Novemba hadi Machi. Aidha, Kisiwa hiki kinaweza kufikiwa kwa kutumia barabara, maji na ndege.

Karibuni sana Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Rubondo. 
MNRT