Kagasheki ateua wajumbe wapya 10 kamati ya ushauri wa ugawaji wa vitalu vya utalii nchini, yumo Zakhia Meghji

PICHANI: Kamati ya Ushauri ya Ugawaji wa Vitalu vya Utalii ikiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi Khami... thumbnail 1 summary
PICHANI: Kamati ya Ushauri ya Ugawaji wa Vitalu vya Utalii ikiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi Khamis Suedi Kagasheki (mwenye kaunda suti) na Kaimu Katibu Mkuu, Bw. Ibrahim Mussa (wa kwanza kulia)

Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Balozi Khamis Suedi Kagasheki amezindua rasmi Kamati ya Ushauri ya Ugawaji wa Vitalu vya Utalii nchini.
Kamati hiyo inaundwa na wajumbe 10 kutoka sekta mbalimbali inajukumu la kumshauri waziri katika masuala yote yalioainishwa kwenye sheria na kanuni za Wanyamapori juu ya ugawaji vitalu.
Akizungumza katika uzinduzi huo uliofanyika katika Ukumbi wa Selous uliopo Wizara ya Maliasili na Utalii Makao Makuu, Dar es Salaam, Mhe. Kagasheki alisema anaimani kamati hiyo itamsaidia kwa kumpa ushauri utakaokuwa umefanyiwa utafiti wakina kutokana na kamati hiyo kuundwa na watu wenye uweledi na uzoefu mbalimbali katika masuala ya usimamizi wa raslimali na maliasili.
Aidha, Mhe. Kagasheki aliwataka wajumbe wa kamati hiyo kutekeleza majukumu waliopewa kwa kushirikiana kikamilifu na kwa kuzingatia maslahi ya taifa.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Ushauri wa Ugawaji wa Vitalu, Prof. Leticia Rutashobya alimshukuru Mhe. Waziri kwa kumpa jukumu la kuongoza kamati hiyo na kuahidi kuhakikisha inatekeleza majukumu yake kwa uadilifu.
Kamati ya Ushauri wa Ugawaji wa Vitalu inaundwa na Prof. Leticia Rutashobya (mwenyekiti) na wajumbe wake Mhe. Zakhia Hamdan Meghji, Bw. Alli Mufuruki, Bw. Mohamed Abdukadir, Bw. Raymond Mbilinyi, Dkt. Simon Mduma, Bw. Allan Kijazi, Dkt. Fred Manongi, Prof. Alexander N. Songorwa na Bi. Agnes Ndumati; na itahudumu hadi tarehe 15 Julai, 2016.