Maadhimisho ya sikukuu ya Utalii Duniani Kitaifa 2013 kufanyika Mkoani Mwanza kuanzia Septemba 22-29

TAARIFA KWA UMMA Maadhimisho ya sikukuu ya Utalii Duniani Kitaifa Mwaka huu yatafanyika Mkoani Mwanza kuanzia tarehe 22-29/9/201... thumbnail 1 summary
TAARIFA KWA UMMA: SIKU YA UTALII DUNIANI

TAARIFA KWA UMMAMaadhimisho ya sikukuu ya Utalii Duniani Kitaifa Mwaka huu yatafanyika Mkoani Mwanza kuanzia tarehe 22-29/9/2013 Septemba. Kauli mbiu ya maadhimisho hayo mwaka huu ni “Utalii na Maji – Kulinda Hatma yetu (Tourism and Water - Protecting Our Common Future) Shughuli zote za maadhimisho hayo zitafanyika katika uwanja wa Nyamagana.

Pamoja na shughuli mbalimbali zitakazofanyika kutakuwepo pia na maonesho yakiwemo ya utalii, malikale, misitu na masuala ya uhifadhi kwa ujumla, na teknlojia mbalimbali. Aidha kutakuwepo pia safari za kutembelea Hifadhi mpya ya Taifa ya Saanane. Wananchi wote mnaombwa kujitokeza na kushiriki katika maadhimisho hayo.


Utalii uanze kwa Mtanzania mwenyewe.

Imetolewa na:
Mkurugenzi Mwendeshaji