Sanamu
kubwa ya Rais wa zaman wa Afrika Kusini Nelson Mandela inazinduliwa rasmi
septemba 21 mwaka huu huko Washington kwenye eneo ambalo maelfu ya wamarekani
walikusanyika kushinikiza kuachiwa kwa Mandela kutoka gerezani na uhuru wa
Afrika ya Kusini kutoka mikononi mwa makaburu.
Sanamu
hilo lenye urefu wa futi sita limetengenezwa na mchonga vinyago Jean Doyle na litawekwa
nje ya ubalozi wa Afrika Kusini Marekani uliopo kwenye jimbo la Massachusetts.
Sanamu
hilo imetengenezwa kwa mfano wa picha aliyowahi kupiga Mandela wakati wa
kutangaza harakati za uhuru nchini humo Febriari 11, 1990.
Waziri
wa Ushirikiano wa Kimataifa, Maite Nkoana-Mashabane na mwenyekiti wa African
National Congress (ANC) Baleka Mbete watakuwa miongoni mwa watakaoiwakilisha
Afrika Kusini kwenye tukio hilo.
Maofisa
kutoka ikulu ya Marekani nao watakuwepo.