Siku ya tembo kitaifa kufanyika Septemba 22 mwaka huu

Tembo ni miongoni mwa wanyama waliokatika hatari kubwa ya kupotea Tanzania katika miaka michache ijayo endapo hakutakuwa na jitihada za ma... thumbnail 1 summary
Tembo ni miongoni mwa wanyama waliokatika hatari kubwa ya kupotea Tanzania katika miaka michache ijayo endapo hakutakuwa na jitihada za maksudi za serikali, wananchi na wadau wote kwa ujumla za kupambana na vitendo vya ujangili ambavyo vimekuwa vikifanywa na watu wenye nia mbaya na taifa hili.

Lakini elimu hii ya kuhifadhi na kulinda wanyamapori wetu hasa tembo inaweza kutolewa kwanamna ipi? njia rahisi ya kuamsha ari na hamasa kwa wananchi wote kushiriki katika mapambano haya ni kuwashirikisha wananchi katika shughuli mbalimbali za uhifadhi huo.

Kwa kuona umuhimu huo Wizara ya Maliasili na Utalii imeandaa maadhimisho ya siku ya tembo kitaifa ambayo yatafanyika siku ya Jumapili ya Septemba 22 mwaka huu ikiongozwa na kauli mbiu “JIUNGE KATIKA MAPAMBANO DHIDI YA UJANGILI WA TEMBO”

Maadhimisho hayo yataanza kwa maandamano yakitokea Chuo Kikuu cha Dar es Salaam majira ya saa mbili asubuhi na kuhitimishwa kwenye ukumbi wa Mlimani City. 

Mara nyingi wananchi wanashindwa kutetea rasilimali zao kutoka na kutokuwa na uelewa wa kutosha juu ya rasilimali hizo lakini utawezaje kujua umuhimu na thamani ya rasilimali hizo kama hushiriki kwenye matukio kama haya? ni fursa nzuri ya kuonyesha uzalendo wako kwa kushiriki katika maadhimisho hayo.