Video: Uoto wa asili wa Tanzania wamvutia mzee wa Azonto-Fuse ODG, ajiona mwenye bahati kuitembelea Tanzania

Hitmaker wa Azonto na Antenna, Fuse ODG ameisifia Tanzania na kusema ina uoto wa asili wa kuvutia na amejisikia raha na fahari kuitembele... thumbnail 1 summary

Hitmaker wa Azonto na Antenna, Fuse ODG ameisifia Tanzania na kusema ina uoto wa asili wa kuvutia na amejisikia raha na fahari kuitembelea.


Fuse ODG ambaye kesho atatumbuiza kwenye viwanja vya Ustawi wa Jamii jijini Dar es Salaam, amesema hayo kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika Hyatt Kilimanjaro Hotel.
“Lengo langu ni kuuonesha upande mwingine nje ya Africa jinsi ilivyo nzuri, nchi kama Tanzania, ina uoto mzuri wa asili, sio tu Dar es Salaam, Arusha pia ni mji mzuri sana na dunia inapaswa kuona hilo,” alisema.
“Lengo langu napenda nikija kwenye nchi, napenda kuchukua kitu ninachoweza kuionesha dunia, hivyo bila shaka, safari hii ya Dar es Salaam mnaweza kunifundisha kitu na nikirudi niweze kuionesha dunia. Kupitia muziki wangu, naicha dunia ijue kuwa Afrika ni sehemu nzuri kuwepo, hivyo ni heshima kubwa kuwa hapa leo na nasubiria kesho kuungana na watu.”
Katika hatua nyingine, Fuse alipata fursa ya kuongelea interview aliyofanya Chris Brown kwenye kituo cha runinga cha BET miezi kadhaa iliyopita ambapo alisema alijifunza kucheza mtindo wa Azonto nchini Nigeria kupitia Wizkid na kuwafanya wengi waliokuwa wakiangalia show hiyo kuelewa asili ya aina hiyo ya uchezaji ni Nigeria.
“Nadhani ilikuwa kosa ambalo Chris Brown alifanya hata Wizkid amesema yeye mwenyewe nilikuwa naye Ghana miezi michache iliyopita. Azonto ilianzia Ghana, Wizkid kama shabiki wake alitengeneza wimbo kuihusu.”
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Times Radio FM, Rehule Nyaulawa, ambaye kituo chake kimemleta msanii huyo, amesema waliamua kumletea Fuse ODG kwakuwa redio hiyo imejikita kupromote muziki wa Kiafrika na kwakuwa nyimbo za msanii huyo zimekuwa zikiombwa sana kwenye vipindi vyao.
Katika show ya kesho, Fuse atasindikizwa na wasanii mbalimbali wa Tanzania wakiwemo Banana Zorro, H. Baba, Snura, Wakali Dancers, Mapacha, Magenge ya Mwenge, Dogo Janja, Tunda Man, Madee, Vanessa Mdee, Mabeste, Gosby, Deddy, Menina, Walter Chilambo, Wakazi

Chanzo: Bongo5