Wasanii wanaweza kukuza sekta ya utalii kwa kufanya kama alichokifanya Diamond Platnumz huko Malaysia

Watu maarufu au wenye majina makubwa kama wanamuziki na waigizaji wananjia nyingi sana za kuingiza kipato chao karibuni katika kila wanachok... thumbnail 1 summary
Watu maarufu au wenye majina makubwa kama wanamuziki na waigizaji wananjia nyingi sana za kuingiza kipato chao karibuni katika kila wanachokifanya, huenda bado hujanielewa ninachokimaanisha lakini kupitia picha za Diamond Platnumz alizoweka kwenye mitandao ya kijamii akionyesha chumba katika hoteli aliyofikia kwenye show yake huko Malaysia imenifanya nilizungumze hili.

Diamond katika picha hizo alizoshare kwa mashabiki wake ambazo ninaamini aliweka tu bila kujua alikuwa akitangaza hoteli hiyo jambo ambalo pengine wasanii wangeanza kulitumia kama biashara angeweza kulipwa kwa kushare picha hizo kwa mashabiki wake.

Unadhani ni watu wangapi sasa watapenda kufikia kwenye hoteli hiyo ambayo Diamond kafikia huko Malaysia? 


Diamond aliweka picha hizo zikiambatana na maneo haya: "Pichani ni chumba cha hotel ninamopumzishia mbavu zangu Tayari kabisa kwa kwa kuwapa watu wangu wa Malaysia burudani  inayowastahili pamoja na kuiwakilisha nchi yangu Tanzania ''

"I hope mashabiki wangu tayari mnafahamu kuwa nimo nchini Malaysia kwa Tour ya kimziki,nashukuru Mungu nilifikia  salama kabisa mimi na team yangu ya WCB WASAFI, nimepata mapokezi mazuri kiukweli kiasi cha kujiskia niko nyumbani"