Fastjet yazindua rasmi safari zake za ndege kati ya Dar es Salaam na Mbeya

Shirika la ndege lenye bei nafuu la fastjet leo limeandika historia mpya kwa kuzindua safari yake mpya ya Dar es Salaam-Mbeya ambayo itak... thumbnail 1 summary
Shirika la ndege lenye bei nafuu la fastjet leo limeandika historia mpya kwa kuzindua safari yake mpya ya Dar es Salaam-Mbeya ambayo itakuwa ikifanyika mara tatu kwa wiki.

Nimekuletea picha mbalimbali za matukio ya uzinduzi wa safari hiyo ambayo mgeni rasmi alikuwa ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Shaban Mwinjaka ambaye aliongozana na Kaimu Mkurugenzi wa Mipango na Sera wa wizara hiyo, Aunyisa Meena na Mkurugenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwl Julius Nyerere (JNIA), Moses Maliki.

 Abiria wakipanda kwenye ndege
Injinia Remigius Mussa, mmoja wa abiria waliokuwa kwenye safari ya kwanza ya fastjet kutoka Dar es Salaam kwenda Mbeya
 Abiria
Wananchi wakiwa wamekusanyika nje ya uzio wa uwanja wa ndege wa Songwe jijini Mbeya ili kushuhudia uzinduzi wa safari za ndege za fastjet mkoni humo


Mkurugenzi uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwl Julius Nyerere (JNIA), Moses Maliki
Meneja uwanja wa ndege wa Songwe jijini Mbeya, Valentino Kadeha
Meneja Mauzo wa fastjet, Vishal Choudry
 Wadau wa usafiri wa anga
Commercial manager wa fastjet, Jean Uku akijadiliana jambo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dr. Shaban Mwinjaka.
Ndege ya fastjet ilipotua tu kwenye uwanja wa ndege wa Songwe ikapigwa 'water Splash', eeh kwa lugha yetu ya kitaalamu yaani ikimaanisha kupewa baraka zote.

 Ndege ya fastjet kwenye uwanja wa ndege wa Songwe
Commercial Manager wa fastjet, Jean Uku, (kushoto)  pamoja na Mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa safari ya Dar es Salaam Mbeya,  Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dr. Shaban Mwinjaka (wa pili kushoto), akifuatiwa na Meneja wa Uwanja wa ndege Songwe, Valentino Kadeha na Meneja Mauzo wa fastjet, Vishal Choudry.

Afisa Mahusiano na Masoko wa Fastjet, Lucy Mbogoro 
 Wageni waalikwa
Meza Kuu: Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwl Julius Nyerere (JNIA), Moses Maliki, Commercial Manager wa fastjet, Jean Uku, Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dr. Shaban Mwinjaka, na Kaiumu Mkurugenzi wa Mipango na Sera kutoka Wizara ya Uchukuzi, Aunyisa Meena.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dr. Shaban Mwinjaka akizindua rasmi safari za ndege ya fastjet kati ya Dar es Salaam na Mbeya
Mgeni rasmi ambaye ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dr. Shaban Mwinjaka akikata keki kuashiria kuzindua safari za fastjet kati ya Dar es Salaam na Mbeya, kushoto ni Commercial Manager wa fastjet, Jean Uku 
Commercial Manager wa fastjet, Jean Uku akimlisha keki mgeni rasmi Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dr. Shaban Mwinjaka
 Commercial Manager wa fastjet, Jean Uku akifafanua jambo
Mwandishi Mwandamizi wa Blog ya Mbeya Yetu, Joseph Mwaisango
Mie mwenyewe hapo
Ndege ya fastjet ikiondoka uwanja wa ndege Songwe, Mbeya

Show nzima ya tukio ilisimamiwa na Mbeya Yetu, kaa standby kupata simulizi nzima ya safari hii ya kwanza ya fastjet kutoka Dar es Salaam Kwenda Mbeya, kupitia mtandao huu.