Mpiga picha za wanyamapori amejikuta katika wakati mgumu baada ya chui kupanda juu ya Land rover aliyokuwa amepanda.
Sergey Kotelnikov
alishtuka sana na kuonekana mwenye uoga mwigi baada ya mnyama huyo
kuruka juu ya gari lake wakati akiwa kwenye safari ya kitalii mpakani
mwa Namibia na Botswana.
Lakini
cha ajabu chui yule hakuwa na madhara maana baada ya kupanda juu ya
gari aliketi na kupiga posi kana kwamba anamwambia mpiga picha huyo
"Nipige picha basi"
Na
baadae yeye na wapiga picha wengine waliungana na kuanza kucheza na
chui yule, ama kweli animal loves human though human do not love them.
Pata mlolongo wa tukio hilo la kusisimua
Hapo anajibaraguza, full uoga na sala za kufa mtu, najua hapa mungu alikuwa bize sana kupokea sala zake
Uuuh! mpiga picha anashusha pumzi baada ya chui kuweka posi akitaka kupigwa picha in a proper way.
Playtime, umemaliza kunipiga picha sasa ngoja nikufundishe michezo yetu ya mwituni
Mama yake chui huyu akitokea hapo sijui itakuwaje
Hakika
kusafiri ni kujifunza, kuna mengi yanatokea hata katika hifadhi zetu
hapa nchini Tanzania, tutembelee maeneo haya ili kujifunza mengi. Picha
na Caters News Agency