UTABIRI WA HALI YA HEWA KWA SAA 24 ZIJAZO KUANZIA SAA 3.00 USIKU WA LEO TAREHE 28/03/2014

WIZARA YA UCHUKUZI MAMLAKA   YA HALI YA HEWA S.L.P.3056, DAR-ES-SALAAM Fax: 2460735. email: met@meteo.go.tz UTABIRI WA HALI Y... thumbnail 1 summary

WIZARA YA UCHUKUZI
MAMLAKA  YA HALI YA HEWA
S.L.P.3056, DAR-ES-SALAAM
Fax: 2460735. email: met@meteo.go.tz

UTABIRI WA HALI YA HEWA KWA SAA 24 ZIJAZO KUANZIA SAA 3.00 USIKU WA LEO.
            TAREHE 28/03/2014.


[Mikoa ya Mara, Mwanza, Kagera, Shinyanga na Lindi]:
[Mikoa ya Mtwara, Ruvuma Mbeya, Iringa na  Rukwa]:
[Mikoa ya Tanga, Pwani , Dar es salaam na Morogoro  ]:
[Visiwa vya Unguja na Pemba]:

Hali ya Mawingu, mvua na ngurumo katika maeneo mengi na vipindi vifupi vya jua.
[Mikoa ya Arusha, Kilimanjaro na Manyara]:
[Mikoa ya Singida na Dodoma]:
[Mikoa ya Tabora na Kigoma]:

Hali ya Mawingu, mvua na ngurumo katika baadhi ya maeneo na vipindi vifupi vya jua.

ANGALIZO

  1. VIPINDI VIFUPI VYA MVUA KUBWA VINATARAJIWA KATIKA MAENEO YA UKANDA WA ZIWA VICTORIA,  MWAMBAO WOTE WA PWANI, NYANDA ZA JUU KUSINI MASHARIKI NA NYANDA ZA JUU KASKAZINI MASHARIKI.
  2. UPEPO MKALI KWA VIPINDI VIFUPI UNAOFIKIA KM 30-40 KWA SAA UNATARAJIWA KATIKA BAADHI MAENEO YA UKANDA WA PWANI. TAFADHALI CHUKUA TAHADHARI.

VIWANGO VYA JOTO, MAWIO NA MACHWEO YA JUA KWA BAADHI YA MIJI HAPA NCHINI:


MJI
Kiwango cha juu cha joto
Kiwango cha chini cha joto
Mawio (Saa)
Machweo (Saa)
ARUSHA
26°C
16°C
12:39
12:44
D'SALAAM
32°C
23°C
12:28
12:33
DODOMA
29°C
17°C
12:42
12:47
KIGOMA     
28°C
21°C
01:06
01:11
MBEYA
24°C
15°C
12:51
12:56
MWANZA
28°C
18°C
12:53
12:58
TABORA
29°C
18°C
12:54
12:59
TANGA
32°C
24°C
12:29
12:34
ZANZIBAR
31°C
23°C
12:28
12:33

Upepo wa Pwani: Unatarajiwa kuvuma kutoka Kaskazini- Mashariki kwa kasi ya km 30 kwa saa kwa Pwani ya
                        Kaskazini na kutoka Kaskazini- Magharibi kwa kasi ya km 30-40 kwa saa kwa Pwani ya Kusini.      
                                                        
Hali ya bahari: Inatarajiwa kuwa na Mawimbi Madogo.

Matazamio kwa siku ya Jumapili: 30/03/2014: Mabadiliko kidogo.  

 Utabiri huu umetolewa leo tarehe 28/03/2014.

Na: MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA.