Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mheshimiwa Ummy Mwalimu afanya ukaguzi wa mazingira viwandani

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mheshimiwa Ummy Mwalimu amefanya ziara ya ukaguzi wa mazingira katika kiwanda cha OK Plastic kilic... thumbnail 1 summary
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mheshimiwa Ummy Mwalimu amefanya ziara ya ukaguzi wa mazingira katika kiwanda cha OK Plastic kilichopo jijini Dar Es Salaam. Ziara hiyo ni muendelezo wa ziara za kuangalia hali ya mazingira kwenye viwanda mbalimbali hapa Nchini.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mheshimiwa Ummy Mwalimu akipata maelezo ya uendeshaji wa kiwanda cha OK Plastic kutoka kwa Menejimenti ya kiwanda hiko.Wengine wanaofuatia ni Mkurugenzi Msaidizi-Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais bi Magdalena Mtenga, Bwana Anacleto Pereira Mkuu wa Idara ya sheria wa OK plastic, Fadl Ghaddar Mkurugenzi Mtendaji wa OK plastic na Martin Msamba Meneja wa kiwanda.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mheshimiwa Ummy Mwalimu akimsikiliza Mkurugenzi Msaidizi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Bi Magdalena Mtenga wakati wa ziara hiyo.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mheshimiwa Ummy Mwalimu akiangalia jinsi betri chakavu zinavyohifadhiwa kiwandani hapo.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mheshimiwa Ummy Mwalim akielekeza jambo wakati wa ziara ya kutembelea kiwanda cha OK Plastic kilichopo jijini Dar Es Salaam