Waziri Makamba ateta na watumishi wa idara ya mazingira

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba hii leo amekutana na Wafanyakazi wa Idara ya Mazingira ka... thumbnail 1 summary
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba hii leo amekutana na Wafanyakazi wa Idara ya Mazingira katika Ofisi yake na kuwataka kufanya kazi kwa weledi na kuandika maandiko mbalimbali ili kupata fedha za kuratibu miradi ya mazingira nchini.
Waziri Makamba amewataka watumishi hao kuacha kufanya kazi kwa mazoea bali kujenga dhana ya uwajibikaji kwa kila mmoja ili kuacha alama kwa yale mazuri yanayofanywa ili iwe kumbukumbu kwa vizazi vya sasa na vizazi vijavyo.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akiongea na watumishi wa Idara ya Mazingira katika Ofisi yake (hawapo pichani). Kushoto ni Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Mbarak Abdulwakil.
 Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais (kulia) akiwa katika kikao kazi kati ya Idara ya Mazingira na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Mazingira Bw. Richard Muyungi.
 Sehemu ya Watumishi kutoka Idara ya Mazingira wamkimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba (hayupo pichani) katika kikao kazi kilichofanyika Mtaa wa Luthuli jijini Dar es Salaam.
Waziri Makamba (wa kwanza kulia) akiteta jambo na Katibu Mkuu Bw. Mbarak Abdul Wakil wakati wa kikao na Idara ya Mazingira.