SHINDA SAFARI YA KUTEMBELEA HIFADHI ZA TAIFA NCHINI

Katika kutambua mchango wa Wananchi katika uhifadhi na kupiga vita ujangili wa wanyamapori na sekta ya misitu nchini, Wizara ya Maliasili ... thumbnail 1 summary
Katika kutambua mchango wa Wananchi katika uhifadhi na kupiga vita ujangili wa wanyamapori na sekta ya misitu nchini, Wizara ya Maliasili na Utalii imeamua kuchezesha bahati nasibu ya kutembelea hifadhi za taifa.

Bahati nasibu hiyo itachezeshwa katika maonyesho ya Biashara ya Kimataifa ya SABASABA yatakayoanza kufanyika Juni 28 hadi Julai 10, mwaka huu katika viwanja vya Mwalimu Julius.K.Nyerere jijini Dar es Salam.

Katika bahati nasibu hiyo itakayochezeshwa kila siku, washindi mbalimbali watakaopatikana watazawadiwa safari ya kwenda kutembelea Hifadhi ya Mikumi na Saadani na kujionea vivutio mbalimbali vya utalii.

Aidha, zawadi mbalimbali zitatolewa kwa washindi mbalimbali watakaoshiriki katika bahati nasibu hiyo.
Sambamba na hilo Wizara katika kuimalisha utalii wa ndani nchini imeandaa Safari za kila siku za gharama nafuu za kutembelea Hifadhi ya Taifa ya Mikumi na Saadani ambapo mwananchi atagharamia usafiri wa kutoka viwanya vya Sabasaba hadi hifadhini na kurejea siku hiyo hiyo jijini Dar es Salaam.

Wizara inatoa wito kwa wananchi wote kutembelea banda la Wizara ili kupata fursa ya kukutana na wadau mbalimbali wa sekta ya utalii, wanyamapori na mambo ya kale watakaokuwa wanatoa elimu juu ya jambo lolote la sekta husika.