Mfuko
wa Vyombo vya Habari Tanzania katika kukuza Uimara Na kujenga Uhuru wa
Vyombo vya habari na Waandishi wa Habari unatoa mafunzo kwa kwa
Waandishi na wamiliki wa vyombo hivyo Mkoani Lindi ili kuwajengea Uwezo
wa kuomba Ruzuku zinazotolewa na Mfuko huo.
Mafunzo hayo ya Siku moja
yanawezeshwa na Mshauri wa mambo ya Habari ambae pia ni mwandishi
Mkongwe,Bw Ndimara Tegambwage na Meneja wa Vyombo vya Habari vya SJMC
Chini ya Chuo kikuu cha DSM,Bi Edda Sanga Kufuatia awamu ya pili ya
Utoaji Ruzuku hizo toka TMF,Mfuko umeamua kutoa mafunzo hayo ili kutoa
msisitizo katika Uandishi wa Habari za Vijijini,Uwazi na
Uwajibikaji,Utawala bora,Ukimwi,Jinsia na kuwapa sauti za jamii
zilizotengwa ili waandishi waweze kupata habari kwa jamii na habari
zinazogusa jamii.
Katika Mafunzo hayo pamoja na
kuwezesha na wakongwe wa habari pia yamehusisha wanahabari na wamiliki
toka mkoani humo yanayoweshwa na Afisa Mwandamizi wa TMF,Alex
Kanyambo,Afisa Mawasiliano TMF,Japhet Sanga na Bi Raziah Mawanga,,,Afisa
Mafunzo Tmf
Picha na Habari..Mdau Abdulaziz video,Lindi