Na Dkt Noorali T. Jiwaji
Leo Jumapili tarehe 8 Septemba, upande wa magharibi karibu na upeo, utauona Mwezi ukiosogea nafasi yake angani mbele ya macho yako, ukiuangalia kwa saa moja hivi kuanzia baada tu ya machweo, hadi baada ya saa mbili hivi. (angalia picha chini)
Nyota
ya Spika inayoonekana kushoto wa Mwezi mwandamo ipo juu kidogo tu ya Mwezi,
lakini baada tu ya saa moja hivi utaona nyota ya Spika iko chini kidogo ya
Mwezi mwandamo.
Kilichotokea
kihalisi ni kwamba kwa vile Mwezi unatembea kwa kasi kubwa katika mzunguko wake
wakati nyota hasizogei, kihalisi, ni Mwezi uliosogea kupanda juu.
Sayari
zote, pamoja na Mwezi, husogea kutoka magharibi kwenda mashariki ukilinganisha
na nyota, ambazo hazisogei angani kwa vile zipo mbali mno na sisi.