Mchungaji Msigwa apongeza mkakati wa Rais Kikwete wa kukomesha vitendo vya ujangili katika hifadhi za Taifa

Mwenyekiti wa MANET Bw  Zuberi Mwachura  kulia  akieleza mkakati  wa  kupambana na vitendo vya ujangili katika  hifadhi ya Taifa  ya  Ruah... thumbnail 1 summary
Mwenyekiti wa MANET Bw  Zuberi Mwachura  kulia  akieleza mkakati  wa  kupambana na vitendo vya ujangili katika  hifadhi ya Taifa  ya  Ruaha  leo
Mbunge  wa  jimbo la  Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa akifafanua  jambo


 Mgeni  rasmi  katika warsha ya  siku  moja ya  kujadili  vitendo  vya ujangili katika  hifadhi ya Taifa ya Ruaha Mbunge  wa jimbo la Iringa mchungaji  Peter Msigwa ( wa pili kushoto) akiwa na viongozi mbali mbali akiwemo mwenyekiti wa taasisi  iliyoandaa warsha hiyo MANET Bw Zuberi Mwachura  na  viongozi  wengine.
....................................................................


Na  Francis  Godwin Blog, Iringa
MBUNGE  wa  jimbo la  Iringa mjini kupitia chama  cha Demokrasia na maendeleo (chadema)amempongeza Rais  Jakaya  Kikwete kwa mkakati  wake wa kunusuru vitendo  vya ujangili  katika hifadhi  za  Taifa.

Huku  mbunge  huyo akidai  kuwa anawajua  viongozi  mbali mbali na watu maarufu ambao wanaendelea kuendesha  vitendo vya ujangili katika hifadhi ya  Ruaha  Iringa  ikiwa ni pamoja na kulitumia gari la  wagonjwa (Ambulence) kusafirisha  meno ya tembo na atawataja  wahusika  bungeni.

Msigwa  ambae ni  waziri  kivuli  wa wizara ya maliasili na utalii alitoa   pongezi  hizo  leo mjini Iringa wakati wakati akifungua kikao  cha  kujadili vitendo  vya ujangili  katika  hifadhi ya Taifa  ya  Ruaha Iringa iliyoandaliwa na taasisi  isiyo ya  kiserikali ya Mazingira Netwark Tanzania (MANET).

"Awali  ya  yote  napenda kumshukuru  sana Rais Jakaya Kikwete  kwa  kuja na mikakati ya kweli ya  kupambana na vitendo vya ujangili nchini  kwa  kutumia askari  wa jeshi la lawanchi Tanzania (JWTZ)...huu ni mkakati  mzuri ambao  binafsi  nimempongeza  sana kwa  hatua  hiyo" alisema Msigwa 

Kuwa  ni mara  kadhaa watanzania  wamepata  kusikia viongozi wa Serikali wenye dhamana wakisema kuwa mtandao wa majangili na wafanyabiashara haramu wa wanyamapori ni mpana na mgumu kuumaliza

Pia ni mara  kadhaa pia Serikali imeendelea kukiri kuwa mtandao huu unawahusisha Wafanyabiashara wakubwa, Wanausalama, Wabunge, Wanasiasa na watu wenye dhamana ya uongozi katika taifa letu umekuwa ni  kikwazo  kikubwa katika  vita dhidi ya ujangili.

“….Serikali imeendelea kutoa matamko kuwa itawataja wahusika wa biashara haramu dhidi ya wanyamapori na kuwachukulia hatua lakini cha kushangaza, mara zote hakuna hatua yoyote inayochukuliwa..ni jambo moja la msingi ambalo ningependa kulizungumza na kusisitiza hapa leo ni juu ya wajibu wa kila Mtanzania katika kuhakikisha kuwa tunaungana kwa pamoja katika vita dhidi ya biashara haramu ya wanyamapori 

Hivyo  alisema hatua ya  Rais  Kikwete  kuweka mkakati  huo wa  kutumia  askari  wa JWTZ katika kulinda  hifadhi  na kupambana na majangili  ni  jambo la kumpongeza.

Kwani  alisema baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere katika tamko lake maarufu mwaka 1961 lijulikanalo kama Arusha Manifesto alisema yafuatayo:
  Uhai wa wanyamapori ni jambo muhimu na linalotuhusu sana sisi sote barani Afrika. Viumbe hawa wa porini, wakiwa   katika mapori wanamoishi,sio muhimu tu kwa ajili ya       kuajabiwa na kuvutia lakini pia ni sehemu ya maliasili yetu na pia ndio mustakabali wa maisha yetu ya baadaye.

Alisema  kuwa mwalimu Nyerere alitambua umuhimu wa kutunza wanyamapori kwa wakati huo tukiwa na hazina kubwa ya wanyama, lakini leo viongozi wa Serikali wameshikwa na kigugumizi katika kuhakikisha dira na jitihada za baba wa taifa letu ,vinatimizwa.

Hivyo  alisema kama kiongozi ambaye wananchi wamenipa dhamana ya kuwawakilisha, nawiwa kutumia nafasi hiyo, kuendeleza juhudi zangu na kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha kuwa kila Mtanzania anakua mdau nambari moja wa kupinga biashara haramu ya wanyamapori kwani si tu kuwa inalitia hasara taifa letu bali pia inaweka hatarini maisha ya wanyamapori kwa vizazi vijavyo.

“Nachukua nafasi hii kuikumbusha na kuitaka Serikali kutimiza wajibu wake kwa kuwafikisha majangili na wafanyabiashara haramu wa wanyamapori katika vyombo vya dola na watendewe ipasavyo kwa mujibu wa Sheria”


Kuhusu  watu  maarufu mkoani Iringa  wanaojihusisha na biashara ya  pembe  za ndovu na hata  kutumia magari ya  umma kama Ambulence  kusafirisha pembe hizo  za ndovu  alisema kuwa ana idadi  yao ndevu zaidi na kuwa katika kikao cha bunge  kijacho ataweka hadharani majina yao.

Chanzo: Mzeewamatukio