Video: Baada ya kuwekwa katikati ya mamba na kundi la mbwa mwitu, Ngiri achagua bora kuliwa na mamba kuliko mbwa mwitu

Kifo bana achana nacho, wakati mwingine kinakuja kwa majaribu sana, ngiri aliyekwenda kunywa maji kwenye bwawa mambo yalimwendea vibaya baad... thumbnail 1 summary
Kifo bana achana nacho, wakati mwingine kinakuja kwa majaribu sana, ngiri aliyekwenda kunywa maji kwenye bwawa mambo yalimwendea vibaya baada ya kugundua kuwa kulikuwa na kundi la mbwa mwitu 10 waliokuwa wakimsubiri amalize kunywa maji ili wamfanya kitoweo. 

Hiyo ndio sababu iliyomfanya atulie muda mrefu majini akishindwa kutoka nje ya maji lakini kumbe kwenye maji hayo kulikuwa na mamba nao walikuwa wakimwinda, yaani we acha tu, alichokifanya ni kupiga mahesabu ya haraka, wapi panaafadhali, kwa mbwa mwitu au kwa mamba, lakini wakati akitafakari hilo, mara ghafla mamba akamkamata na kumtupa kwenye maji...., tazama video yake..