Wadau waiomba Serikali kuacha kutaja thamani ya meno ya tembo

SERIKALI imeombwa kuharamisha utajaji wa thamani ya meno ya Tembo yanayokamatwa kote nchini ikiwa ni njia mojawapo ya kupambana na ongezeko... thumbnail 1 summary
SERIKALI imeombwa kuharamisha utajaji wa thamani ya meno ya Tembo yanayokamatwa kote nchini ikiwa ni njia mojawapo ya kupambana na ongezeko la ujangili na biashara ya nyara hizo sa Serikali.

Ombi hilo limo katika maadhimio mbalimbali ya wadau waliokuwa wanajadili namna ya kupambana na ujangili majadilano ambayo yamefanyika Mjini Iringa na kuandaliwa na Mtandao wa Mazingira nchini (MANET).

Mapendekezo mengine yaliyomo kwenye maadhimio hayo ni pamoja na ombi kwa Serikali iwe inalipa fidia halali kwa mazao yanayoharibiwa na wanyamapori ili kuepusha watu kuwachukia wanyamapori hao na pia sheria ya kupambana na ujangili irekebishwe kwa sababu imepitwa na wakati na ndiyo imekuwa chanzo cha kushamiri kwa ujangili nchini.

Akisoma maadhimio hayo ambayo yatapelekwa Serikalini na Mtandao huo wa Mazingira nchini MANET,Mwenyekiti wa Mtandao huo,Bw.Zubery Mwachulla amesema wanawarsha wanaona kuwa utajaji wa thamani ya meno ya tembo kila yanapokamatwa imekuwa ni kichocheo cha kuongezeka kwa ujangili nchini

Naye Mratibu wa Mradi wa Kuboresha Mtandao wa maeneo yaliyohifadhiwa kusini mwa Tanzania (SPANEST),Bw.Godwell ole Meing'ataki amesema ni wakati sasa wa kuanza kufikiria visivyofikirika ikiwemo kubadili utamaduni wa kufanya doria mchana na kuanza kufanya doria hizo usiku ili kupambana na ujangili.


Mwenyekiti wa Kikosi Kazi cha kupambana na ujangili katika vijiji vinavyozunguka hifadhi ya Taifa ya Ruaha,ambaye pia ni Diwani wa kata ya Ilolompya,Mh.Fundi Mihayo amesema majangili wanafahamika lakini wanaogopwa kwa sababu mbalimbali ikiwemo uwezo wao kifedha.