Warsha kuhusu kuenea kwa hali ya jangwa na ukame na maendeleo endelevu ya ardhi yaanza mjini Bagamoyo

Sehemu ya wajumbe wa warsha ya  mafunzo kuhusu kuenea kwa hali ya  jangwa na ukame na maendeleo endelevu ya ardhi mjini  Bagamoyo wakiskl... thumbnail 1 summary
Sehemu ya wajumbe wa warsha ya  mafunzo kuhusu kuenea kwa hali ya jangwa na ukame na maendeleo endelevu ya ardhi mjini Bagamoyo wakiskliza hotuba iliyokuwa ikitolewa na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Injinia Angelina Madete
 Kaimu Mkurugenzi wa mazingira ofisi ya Makamu wa Rais bibi
Magdalena Mtenga akimkaribisha mgeni Rasmi Injinia Angelina
Madete aweze kufungua warsha ya mafunzo kuhusu kuenea kwa
hali ya jangwa na ukame na maendeleo endelevu ya ardhi mjini
Bagamoyo
 Naibu Katibu Mkuu  Ofisi ya Makamu wa Rais Injinia Angelina
Madete akifungua warsha ya siku mbili kwa wafanyakazi kutoka
sekta mabalimbali za Serikali juu ya mafunzo kuhusu
kuenea kwa Hali ya jangwa na ukame na maendeleo endelevu ya
ardhi mjini Bagamoyo leo
Wajumbe wa warsha ya mafunzo kuhusu kuenea kwa hali ya
jangwa na ukame na maendeleo endelevu ya ardhi mjini
Bagamoyo leo wakiwa katika picha ya pamoja na Mgeni rasmi
katika warsha hiyo Injinia Angelina Madete


Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Injinia Angelina Madete amesema ukame umekuwa tatizo kubwa linaloleta athari katika swala zima la mazingira katika nchi zinazoendelea ikiwamo Tanzania.
Inakadiriwa kuwa aslimia 73 ya nchi za Afrika zimepunguza uwezo wa kuzalisha chakula kunakotokana na ukame jambo linalosababisha kuwepo upungufu mkubwa wa chakula. 
Madete ameyasema hayo leo mjini Bagamoyo  wakati wa  ufunguzi wa warsha ya  siku mbili kuhusu kuenea kwa hali ya jangwa na ukame wa maendeleo endelevu ya ardhi.
Alitaja baadhi ya mikoa iliyoathiriwa na ukame ambayo ni Dodoma, Singida na maeneo machache ya mikoa ya Shinyanga, Mara, Iringa, Manyara na Arusha.
Warsha hiyo imewashirikisha wafanyakazi kutoka wizara mbalimbali za Serikali kwa lengo la kuwaongezea uelewa juu ya umuhimu wa utunzaji wa mazingira kwa lengo  kuepuka  janga la ukame.
Akiongea katika warsha hiyo Injinia Madete alisema  kuwa ukame unaleta umaskini na pia ukame umechangia wananchi wengi kuhama maeneo yao na kwenda sehemu zingine zisizo na ukame.
Aliendelea kusema kuwa Serikali imechukua hatua mbalimbali kukabiliana na swala hilo la ukame amabapo mwaka 1994 ilisaini Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Kupamabana na kuenea kwa hali ya jangwa na ukame (United Nations Convetion to Combat Dessertification UNCCD)
Serikali inatekeleza mkataba huo kupitia Programu ya Taifa ya kupambana na kuenea kwa hali ya Jangwa na ukame (National Action Programme to Combat Dessertification-NAP) ambapo kususdi kubwa la mkataba huu ni kuimarisha maisha ya kila siku ya mwananchi wa kawaida aishiye kwenye sehemu za Ukame.

Warsha hiyo ya siku mbili imewashirikisha pia wadau wa mazingira kutoka sehemu mbalimbali wakiwemo wafadhili kutoka Shirika la Maendeleo la Umoja Wa Mataifa (UNDP)

Picha na Habari na Monica Sapanjo
Afisa Habari
Ofisi ya Makamu wa Rais